RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA RAIS XI JINGPING WAPONGEZWA CHINI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa idara ya mambo ya nje ndugu Liu Jianchao ambaye amesema kuwa CPC na Serikali yake wanatambua juhudi kubwa za kuleta maendeleo zinazofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
katika ,mazungumzo hayo yaliyofanyika beijing China , Agosti 26,2024 Balozi Nchimbi pamoja na kufikisha salamu za Mwenyekiti amesema kuwa Tanzania kwa ujumla wanaichukulia China kama mfano wa kuigwa , chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping CPC imeweza kuiongoza China kupiga hatua za maendeleo makubwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.