BALOZI NCHIMBI ASHIRIKI MISA, SHEREHE KUWEKWA WAKFU ASKOFU MSAIDIZI KIBOZI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, Mei 12, 2024, ameshiriki misa takatifu na sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Katoliki Dodoma, Padri Wilbroad Henry Kibozi, iliyofanyika katika Kituo cha Hija cha Kanisa Katoliki, Miyunji, Mbwanga, jijini Dodoma.