NAIBU KATIBU MKUU TANZANIA BARA AONGOZA KIKAO CHA WATUMISHI WA CHAMA NA JUMUIYA ZAKE MKOA WA MBEYA
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. John V.K. Mongella ameongoza kikao cha Watumishi wa CCM Mkoa na Jumuiya zake Mkoa wa Mbeya
Aidha katika kikao hicho Mongella amewasisitiza Watumisha kufanya kazi kwa umoja na kujiepusha na makundi yasiyo na tija kwa ustawi wa Chama Chetu.
Mongela amewaomba Watumishi wa Chama Mkoani Mbeya kuwa na Uadilifu, Uweledi hasa katika kuwatumikia Wananchi na kutatua Changamoto zao.
Mongela ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Mbeya ameyasema hayo katika ukumbi wa Mkapa leo tarehe 10 Julai 2024.