Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


CCM ITAENDÈLEA KUUNGA MKONO SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

alternative

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dk. Emmanuel Nchimbi amesema, Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono uwepo wa serikali ya umoja wa Kitafa ambayo imeimarisha utulivu wa kisiasa visiwani Zanzibar. Dk. Nchimbi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Mamia ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumpokea katika viwanja vya Ofisi kuu za CCM Zanzibar ikiwa ni siku chache mara baada ya kutangazwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Alisema, Chama cha Mapinduzi kina msimamo usiyoyumba kuhusu umoja, utulivu na mshikamano wa nchi na ndiyo maana Chama hicho kitaendelea kuunga mkono uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa.

"Wale ambao wamezaliwa juzi wanaweza wasijui maana ya neno siasa za kihasama, miaka ya 2000 tumeshuhudia siasa za kihasama zilizokuwepo Unguja na Pemba ambapo watu wa familia moja wamenuniana hawaongei mwaka mzima kwa sababu ya siasa za kihasama," alisema.

Hivyo aliwashangaa wale ambao wanaona serikali ya umoja wa kitaifa haina umuhimu ambapo tangu kuanza kwa serikali ya serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar kumekuwa na utulivu mkubwa wa kisiasa.

Alisema, mtu yoyote ambaye anaona serikali ya Umoja wa Kitaifa haina umuhimu basi mtu huyo hajali maisha ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla. "Wewe ukiona mtu ana hamu hamu hivi ya kuona serikali ya umoja wa kitaifa imevunjika basi ujue muda wote anapotembea pua zake zinatamani kunusa damu za watu," alieleza. Hivyo alisema, ni lazima wana CCM waungane na kushirikiana na kwamba msimamo wao usiyumbe na kwa pamoja waune mkono serikali ya umoja wa kitaifa.

Lakini pia aliwaambia watu wa Chama cha ACT kwamba wajue na wao wana wajibu wa kuunga mkono serikali ya umoja wa Kitaifa na kama kuna mambo madogo madogo basi wakae pamoja wazungumze, hiyo ndiyo maana ya maendeleo na ushirikiano.

"Ni lazima tujue wote ni wazanzibari, sote ni watanzania swala la kupendana sisi kama Watanzania ni wajibu wa kiraia," alisema. Hivyo alieleza kuwa, wanaposema wanataka serikali ya umoja wa kitaifa wanataka iwepo wayaseme hayo kwa dhati huku wakijua kwamba wanataka kuendelea kushirikiana na ndugu zao wote.

Alisema, wanatakiwa kuyatekeleza hayo wakiwa na imani ya dhati kwamba wanafanya hivyo wakiwa na nia njema na ni sehemu ya kuyaenzi Mapinduzi.

"Waasisi wa Mapinduzi hawakukusudia kwmaba tuje tuwe na nchi iliyojaa uhasama, tuje tuwe na nchi iliyojaa chuki, isiyo ua umoja, haya hayakuwa matarajio ya waasisi wa nchi yetu, hayakuwa matarajio ya waasisi wa Chama chetu wala hayakuwa matarajio ya waasisi wa Mapinduzi," alise

Hivyo alisema ni lazima wote washirikiane na waziunge mkono serikali kwa kila inavyowezekana kwa lengo kudumisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Aidha alieleza kufurahishwa kwake na maono ya Rais Dk. Mwinyi ya kuendeleza serikali ya umoja wa Kitaifa kwa maslahi mapana ya nchi yao.  

Sambamba na hayo Dk. Nachimbi aliwahakikishia wana CCM kuwa Chama hicho kitaendelea kuimarisha usimamizi wa serikali zake kuhakikisha kwamba serikali zinatimiza wajibu wake wa kutekeleza ilani ya CCM na kuwatumikia wananchi kwa uadilifu mkubwa.

Alisema, kazi wanazozifanya marasi Dk. Samia na Dk. Mwinyi kubwa na kwamba inahitaji wa wana CCM kuspitia chama chao kuimarisha usimamizi wa serikali hizo, na kuwahakikishia watazisimamia serikali chini ya Mwenyekiti wa CCM.

Aidha aliwakumbusha wana CCM juu ya kuvunja makundi kipindi ambacho uchaguzi unamalizika na kupatikana kiongozi aliyevhaguli na wote wanatakiwa kumuunga mkono kiongozi huyo.

"Tunapokwenda kwenye uchaguzi utaanza kumwambia mtu wa kwanza unataka kugombea atakuunga mkono, utamwambia wa pili na watatu nao watakuunga mkono wakati mwegine wanafika 30 mpaka 40 ambapo wakishafika hapo wanaitwa kundi na mwengine naye atafanya hivyo na kila mtu atakuwa na kundi lake ambalo linamuunga mkono," alisema.

Hivyo alieleza kuwa watakapomaliza uchaguzi basi makundi hayo ni lazima yafe, na kusema kuwa mtu akishapakua chakula anauzima moto wake na kwamba ni mjinga pekee anayeendelea kukoleza moto wakati ameshapakua chakula.

Alisema, habari za uchaguzi ni lazima zife na kwamba walioshinda ni lazima wawe wanyenyekevu na walioshindwa ni lazima wajue kama kushinda au kushindwa kupo katika mapenzi ya Mungu.

"Utashindwa leo lakini utashinda kesho, mimi nimegombea nadhani mara 27, nimeshindwa mara sita wala haikuwa shida na ukiwa kama mwanasiasa kushindwa nayo ni raha, na kama hujawahi kushindwa wewe siyo mwanasiasa bwana," alisema DIMWA

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed 'Dimwa' alisema wana CCM wanampongeza Dk. Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa Katubu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.

Alisema, imani hiyo aliyopewa na Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa wanajua kuwa ana uwezo wa kuitumikia nafasi hiyo.

Alisema, kwa mujibu wa Katiba ya CCM ibara ya 15 inasema wajibu wa wanachama ni kujua kwamba chama cha Mapinduzi ndiyo chenye nguvu uwezo wa kwamba nguvu hizo zinatokana na umoja wa wanachama fikra sahihi za CCM na kukubalika kwake na umma.

Hivyo alisema, kulinda na kuendeleza mambo hayo ni wajibu wa kwanza wa kila mwanachama wa CCM, na kusema kuwa wana imani kuwa Dk. Nchini ana uwezo na nguvu za kukiongoza chama hicho kwa mujibu wa katiba ya chama hivho.

Alisema, wana imani kuwa Dk. Nchimbi, atakifikisha chama hicho katika kuleta ushindi wa uchaguzi mkuu uliopo hivi karibuni nchini.

Aidha alisema, anafahamu kuwa Dk. Nchimbi ni Katibu Mkuu wa 11 tangu kuzaliwa kwa CCM ambapo ametanguliwa na watangulizi mbali mbali ambao kijitia amekipokea kutoka kwa Daniel Chongolo.

"Ndugu Katibu Mkuu tunasema karibu katika Chama cha Mapinduzi, tumekupokea kwa mikono miwili na kukupa ushirikiano wa dhati, tutashauriana na wewe, tutafanya kazi kwa pamoja usiku na mchana kuhakikisha chama hichi kinakwenda mbele," alisema.

Mamia ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamejitokeza katika viwanja wa Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi Zanzibar katika hafla ya kumpokea Katibu Mkuu huyo ambaye alifika kwa ajili ya kujitambulisha.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi