Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka kipaombele katika kuwekeza na kuimarisha Ustawi na maendeleo ya Vijana kwa kuweka Sera na Mipango madhubuti kwa lengo la kuharakisha maendeleo yao nchini.
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa Sera ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar ya Mwaka 2023 katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Amesema Serikali inatambua kuwa Vijana ni nguvu kazi na rasilimali ya maendeleo ya Taifa lolote lile ulimwenguni hivyo Serikali imeona umuhimu wa kuweka Sera na Mipango madhubuti kwa Vijana sambamba na kuanzisha Idara, Mabaraza na Jumuiya za Vijana kwa lengo la kuhakikisha maendeleo ya Vijana yanapatikana.
Mhe. Hemed amesema Sera mpya ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2023 imedhamiria kuimarisha na kuwekeza zaidi katika kukuza ustawi na maendeleo ya vijana nchini hasa katika Sekta ya Elimu, Afya, Utawala bora, Uwekezaji, Ajira, Ubunifu, Teknolojia ya Habari ba Mawasiliano (TEHAMA).
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefahamisha kuwa Sera hiyo itajikita katika kuimarisha Mila, Silka, Utamaduni, Sana, Michezo, Ushiriki na ushirikishwaji wa Vijana wakiwemo wenye mahitaji maalum pamoja na kupiga vita dhidi ya UKIMWI, Madawa ya kulevya , Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia pamoja na udhalilishaji.
Sambamba na hayo Mhe Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo ya Vijana nchini imefanikiwa kuimarisha masuala ya Mafunzo na uwezeshaji wa Vijana ambapo jumla ya vijana laki tatu sitini na mbili elfu, mia tisa na mbili(362,902) wameweza kupatiwa mafunzo ya Ujasiriamali, Stadi za maisha, Afya ya uzazi, Uongozi na Uzalendo, matumizi ya TEHAMA na utunzaji wa Amani na Usalama nchini kwa maslahio yao na vizazi vijavyo.
Mapema Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema Sera ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar ya mwaka 2023 itakuwa msaada tosha kwa Wizara katika kuimarisha uratibu na usimamizi wa shuhuli na program za maendeleo kwa ustawi wa Vijana nchini.
Amesema kuwa kupitia Sera hiyo mpya Vijana watajengewa uwezo wa kiutendaji kupitia Baraza la Vijana Zanzibar, Asasi zisizo za Kiserikali na wadau wa maendeleoya kwa maslahi yao binafsi na taifa kwa ujumla.
Mhe. Tabia amesisitiza kuwa Sera ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar italeta tija kwa kuwepo mashirikiano baina ya Vijana, Taasisi za Kiserekali, Asasi za kiraia, washirika wa maendeleo, Taasisi za Kidini, Jamii, wazazi na familia ili kufikia malengo yaliyowekwa ndani ya sera hio.
Kwa upande wake Mkurugnzi Mkaazi kutoka Shirika la USAID Ndg. Stephen Andoseh amesema Shirika la USAID kipaombele chake kikubwa ni kuhakikisha Vijana wanashiriki na kushirikishwa katika ngazi mbali mbali za maamuzi hasa kwa vijana wenye mahitaji maalumu kuona wanapewa kipaombele katika kushiriki mambo ya kijamii, kiuchumi na Kisiasa.
Amesema kuwa kuzinduliwa kwa Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2023 itawasaidia vijana katika kuwajengea mazingira mazuri na wezeshi Vijana wa Zanzibar katika upatikanaji wa Ajira, kuwawezesha kiuchumi, kuwapatia mafunzo ya uwongozi na kuwafundisha namna ya kuzikabili na kuzitatua changamoto zinapotokea.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.