Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
TUMEFURAHISHWA NA MAFUNZO
Viongozi na watendaji wa CCM na jumuiya zake katika Mkoa wa Lindi, wamesema wamefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Chama ya kuwapatia mafunzo ya falsafa, itikadi na sera za CCM .
Wamesema hayo kwa nyakati tofauti, jana Oktoba 16 na leo Oktoba 17, 2023, walipokuwa wakitoa salamu za pongezi kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Ndg. Sophia Mjema, ambaye Idara anayoiongoza ndiyo inayoratibu mafunzo hayo yaliyoanza kutolewa mkoani humo Oktoba 11 hadi 16, 2023.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ndg. Barnabas Esau, amesema mafunzo hayo yamekuwa ni elimu muafaka kwa viongozi na watendaji wa CCM na jumuiya zake.
"Sasa kila mmoja anajua wajibu wake barabara, tunashukuru sana kwa uamuzi wa kutuletea mafunzo mpaka huku ngazi za chini," amesema.
Kiongozi mstaafu, Ndg. Benigno Matei Makwinya, amesema ni miaka mingi imepita tangu kupatiwa mafunzo ya aina hiyo.
Ndg. Makwinya, ambaye ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa mstaafu, na aliwahi kuwa diwani na mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama, amesema enzi za TANU mafunzo kama hayo yalikuwa yakitolewa kwa wanachama.
"Uamuzi huu wa kutoa mafunzo kwa viongozi na wanachama unapaswa kuendelea, toeni mafunzo nchini kote, sisi wanachama wa TANU tulikuwa tunafundishwa," amesema.
Ndg. Makwinya amemtuma Ndg. Mjema kufikisha salamu za shukurani kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kupatiwa mafunzo hayo.
Mapema, Ndg. Mjema alisema mafunzo hayo yalizinduliwa mkoani Dar es Salaam na yamepangwa kufanyika nchini kote, ikiwa ni utekelezaji wa moja ya maazimio ya Mkutano Mkuu wa 10 wa CCM uliofanyika 2022.
Ndg. Mjema amesema ni matarajio baada ya mafunzo viongozi na watendaji wa Chama na Jumuiya zake, wataimarika kwa kila mmoja kuelewa kwa ufasaha kazi na majukumu yake ndani na nje ya Chama.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.