Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
WAZIRI BASHE AMTHIBITISHIA BALOZI DKT. NCHIMBI KUWA SERIKALI ITAFUNGUA MAGHALA YA (NFRA) KUANZA KUNUNUA MAZAO KWA WAKULIMA
> Asema ruzuku ya mbolea kuendelea kutolewa kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
> Asema wizara inatekeleza agizo la Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi kulipa madeni ya nyuma ya wakulima.
> Abainisha kuwa serikali imepiga marufuku vyama vya ushirika kukoa fedha kwakuwa mzigo wanaangushiwa wakulima pasipo kushirikishwa katika hatua za ukopaji wa fedha hizo
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amempigia simu Waziri wa Kilimo Ndugu. Hussein Bashe na kumtaka kutolea ufafanuzi kuhusu suala la changamoto ya mahindi ya msimu uliyopita ambayo bado yapo kwenye (store) zao wakulima kwakuwa hayajanunuliwa hadi sasa na msimu mpya unaenda kuanza jambo litakalopelekea kuwa na mahindi mengine hivyo ombi lao kwa serikali ni kuona namna gani itawasaidia kuhakikisha wanapata soko la mahindi yao.
Akizungumza kwa njia ya simu kwenye mkutano wa hadhara Mbinga Mkoani Ruvuma, Waziri Bashe ameanza kwa kusema kuwa Wizara ilipokea maelekezo yake Katibu Mkuu ya kulipa madeni ya msimu huu uliobaki walipokuwa wakinunua na kumueleza kuwa kwa sasa wapo hatua ya mwisho kumaliza kulipa madeni hayo na kuwahakikishia wakulima wote wa Mbinga na Ruvuma kwa ujumla na mikoa yote ya kilimo cha mahindi nchini kwamba serikali itafungua tena maghala NFRA (wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula) kama walivyonunua mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu itanunua mahindi kwa bei nzuri na kuwataka kutoa hofu katika hilo.
Pia, Waziri Bashe amesema baada ya bajeti kupita mwezi wa 5 mwaka huu, wizara itatangaza tarehe ya NFRA kuanza kununua mahindi yakiwemo ya mwaka jana waliyobaki nayo.
Vilevile , Waziri Bashe amemthibitishia Katibu Mkuu kuwa ruzuku ya mbolea kwa wakulima itaendelea vilevile kwa kulingana na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba mpaka 2025/2026 serikali kuendelea kutoa ruzuku ya mbolea kama kawaida.
Aidha, Waziri Bashe amebainisha kuwa wakulima wa kahawa wa Mbinga , katika kikao walichofanya hivi karibuni, amemuelekeza Mrajis wa vyama vya ushirika kwenda kupitia upya mfumo wa vyama vya msingi kukopa fedha kwa niaba ya wakulima na mwisho wa siku mzigo wa madeni unabebeshwa kwa wakulima, kwahiyo watapitia mfumo na serikali imepiga marufuku vyama vya ushirika kukopa fedha halafu mzigo kubambikiziwa wakulima wa wa kahawa bila hata wao kuambiwa.
Bashe ameendelea kusisitiza kuwa serikali inaenda kubadilisha bei wanayobebeshwa wakulima ya kulipia magunia ya kahawa baada ya bunge la bajeti utatangazwa mfumo mpya wa uuzaji wa kahawa.
🗓️22 Aprili, 2024
📍Mbinga - Ruvuma
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.