Wizara ya mambo ya ndai Yapokea Muundo Unaopendekezwa wa Shirika la Polisi
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepokea Muundo Unaopendekezwa wa Shirika la Uzalishaji Mali wa Jeshi la Polisi kutoka kwa timu ya Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiongozwa na Profesa John Kafuku ambapo Shirika hilo la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi lilianzishwa Machi,29,2013 kupitia Agizo la Rais namba 66 la kuboresha miundombinu na kujenga uwezo wa kiuchumi wa Jeshi la Polisi baada yay a Serikali kupitisha Mkakati wa Maboresho wa Jeshi la Polisi wa miaka mitano unaolenga kujenga usasa,ushirikiano wa jamii na utaalamu.
Akizungumza wakati wa wasilisho hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni alisema adhma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuona vyombo vya ulinzi na Usalama vikibakia katika majukumu yake ya msingi ambayo ni ulinzi wa raia na mali zao huku mashirika ya uzalishaji mali yaliyopo katika vyombo hivyo yakiachwa yafanywe shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo,uzalishaji wa fenicha,ushonaji wa nguo,utengenezajai wa viatu.
‘Maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalikua yapo wazi na yalilenga kuyafanya majeshi yetu yawe na mashirika ambayo yako katika ushindani katika sekta husika ikiwa ya kilimo au viwanda na akataka mapato yanayotokana na mashirika hayo yatumike kuimarisha vyombo hivyo vya ulinzi na usalama’.alisema Waziri Masauni Pia amewapongeza wataalamu hao kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa wasilisho la muundo pendekezi huku akiwaomba kujumuisha na maoni yaliyotolewa na wajumbe wa kikao hicho huku akiwaomba kuhakikisha wanarejesha muundo huo wa mwisho ili shirika liweze kuingia kwenye utendaji wa miradi mbalimbali iliyopo mbele yake ikiwemo mradi wa miji salama.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Ally Senga Gugu,Naibu Katibu Katibu Mkuu,Dkt. Maduhu Kazi,Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Kamishna wa Polisi,Liberati Sabas na Wakurugenzi wa Idara zilizopo chini ya wizara hiyo.
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
25-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
25-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
25-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
25-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
25-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
25-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
25-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
25-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
25-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
25-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
25-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
25-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
25-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
25-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
25-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
25-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
25-05-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
25-05-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
25-05-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
25-05-2026