CHONGOLO AMSHITUKIA MKANDARASI KUSUASUA UJENZI WA BARABARA YA KIBAONI-STALIKE MLELE
*Ahoji mkandarasi kukwangua barabara aliposikia ujio wake
*Atoa maelekezo kwa DC ‘kushughulika’ na Mchina anayejenga
*Ang’aka akiwataka watendaji kusimamia fedha za umma kwa uchungu zilete matokeo
Mpimbwe, Mlele, Katavi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Daniel Chongolo ‘amemshtukia’ Mkandarasi anayejenga Barabara ya Kibaoni - Stalike, kwa kiwango cha lami, baada ya kukagua na kushuhudia ujenzi wa barabara hiyo ukisuasua na kuwa nyuma ya muda, kinyume cha mkataba.
Kufuatia hali ya kusuasua kwa ujenzi wa barabara hiyo muhimu inayotarajiwa kuufungua zaidi Mkoa wa Katavi kuunganisha na mikoa mingine ya jirani na kuchochea zaidi shughuli za uchumi na uwekezaji wa wananchi wa maeneo hayo, ametoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya ya Mlele, Majid Mwanga, kukutana na uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mshauri Mwelekezi na Mkandarasi CSRG ili kuhakikisha kasi ya ujenzi inaongezeka kulingana na mkataba.
Chongolo ametoa maelekezo hayo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo iliyopo wilayani Mlele, Katavi Oktoba 4, 2023, akiendelea na ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020 - 2025 na kusikiliza changamoto za wananchi.
“Wakati wa kuhitimisha ziara yangu Oktoba 7, 2023, atakuja Waziri wa Ujenzi. Nimemuita tukutane Mpanda hapo, aje mwenyewe kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kuwaeleza wananchi ni namna gani barabara hiyo itakamilishwa kwa kasi inayotakiwa,” amesema Komredi Chongolo.
Barabara hiyo yenye urefu wa zaidi ya Km 50 itakayogharimu zaidi sh. Bil. 80, inajengwa na Kampuni ya China ya CRSG. Ujenzi wa barabara ulianza Juni 23, 2022 na unatarajiwa kukamilika Juni 22, 2025.
Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa CCM, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo, Kaimu Meneja wa TANROADS, Mkoa wa Katavi, Albert Laizer amesema kuwa hadi sasa umefikia asilimia 11.2 nyuma ya utekelezaji ambao ulipaswa uwe asilimia 21. Muda umefika miezi 15 kati ya 36 iliyopangwa. Na hadi sasa mkandarasi huyo ameshalipwa malipo ya awali zaidi ya sh. Bil. 12.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025