Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


DK. MWINYI AMEMALIZA ZIARA ZAKE UNGUJA

alternative

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ameitaja mikakati mitano ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika kujiandaa kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 kwa kuhakikisha inashika dola kwenye uchaguzi huo.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na mabalozi wa CCM katika ukumbi wa mkutano wa CCM Mahonda uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais Dk.Mwinyi alisema CCM ina wajibu wa kujiandaa kuendelea kushika dola kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.

"Sasa nini tufanye la kwanza kabisa ni kutoa mafunzo kumekuwa na viongozi wengi wapya waliochaguliwa katika uchaguzi wa ndani ya chama hivyo kwa makusudi lazima tufanye mafunzo kwa viongozi wa ngazi zote,"alisema

Alisema akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar atahakikisha anatafuta uwezeshaji ili mafunzo ya anze kwa viongozi wote wa ngazi zote ili atambue wajibu wake kwenye majukumu yao.

"Na mimi nataka kusema wajibu huu ni kwa viongozi wa ngazi za juu tu bali wajibu huu wa mafunzo ni muhimu zaidi kwa ngazi za chini kwa sababu ndipo walipo wanachama wenyewe hivyo lazima tufanye mafunzo kwa makatibu wetu wa matawi,mashina ili watambue vyema wajibu wao,"alisema

Alisema mkakati wa pili ni kushiriki vikao vya kikatiba kutokana na kuwa kuna wakati mwingine vikao hivyo havifanyiki na kwamba endapo vikao hivyo visipo fanyika chama hakitatambua changamoto zilizopo.

"Tusipofanya vikao hatutaona hali chama ipo vipi mbele ya safari hivyo nihimize kwa ngazi zote vikao vya kikatiba vifanyike hii pia ni moja ya mkakati wetu wa chama katika kuhakikisha tunashika dola mwaka 2025,"alisema

Katika maelezo yake Rais Dk.Mwinyi alisema mkakati wa tatu ni kuhakikisha kuwepo kwa madarasa ya itikadi na kwamba hatua hiyo ni njia pekee ya kujenga chama.

"Tusiyazarau hata kidogo Lazima tuhimize madarasa haya ya itikadi yafanyike na kidogo ili wanachama na viongozi wajue wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku,"alisema

Rais Dk.Mwinyi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alisema mkakati wa nne ni kuhakiki daftari la wapiga kura na kwamba kufanya hivyo itasaidia chama kujua nguvu yake.

"Ili ujue nguvu yako lazima ujue una wapiga kura wangapi hivyo daftari la wapiga kura wakati wa kuanza kuhakiki ndio huu kuanzia sasa mpaka kufika kipindi cha uchaguzi tuhakiki vizuri tuhakikishe idadi tuliosema tunayo tunayo kweli tuhakikishe hao wapiga kura wapo kweli,"alisema

Alisema jukumu hilo ni la ngazi zote na kwamba kila mwanachama ana wajibu kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika inavyotakiwa.

"Mkakati mwingine ni kuhimiza ulipaji wa ada za uanachama kutokana na kuwepo kwa mazoea kwamba watu wanasubiri wakati wa uchaguzi wagombea wawalipie ada ili jambo naomba tulikemee na tuhimize watu kulipa ada mwanachama mzuri ni yule anayejitolea kulipa ada kwa pesa yake na haya ndio mambo ya msingi yanayohitajika kwenye rasilimali fedha ,"alisema

Alisema mkakati wa tano ni kuongeza idadi ya wanachama na kwamba chama cha siasa chochote mtaji wake ni wanachama wapya.

"Lazima tuwe na jitihada za kuhakikisha tunaongeza idadi ya wanachama na pia ninatambua kazi nzuri inayofanyika katika maeneo mbalimbali sasa hivi watu wengi wanahamu ya kuingia kwenye chama chetu tutumie nafasi hii kuwaingiza tupate wanachama wapya,"alisema

                            ASISITIZA UMOJA

Rais Dk.Mwinyi alisema baada ya uchaguzi wa chama kumalizika zipo kasoro zilizojitokeza katika chama kutokana na makundi hivyo ni vyema kuachana na makundi hayo ili kukipa ushindi chama wakati wa uchaguzi.

"Tunajua kuwa yapo makundi kwani kina kila aliyemtaka lakini inavyotakiwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi baada ya viongozi wameshachaguliwa basi sote tuvunje kambi zetu na tuwe nyuma ya wale waliochaguliwa," alisema

Alisema hatua ya kuvunja makundi hayo ni kukijenga chama na kufanya kazi ya kukiletea chama cha CCM ushindi wa mwaka 2025.

Mbali na hilo,alisema kazi ya kwanza ya chama cha siasa ni kushika dola, hivyo wanaCCM wanawajibu wa kujiandaa kwa mwaka 2025 kushika dola.

Mapema, Naibu Katibu wa Chama cha CCM Zanzibar, Dk. Mohammed Said Mohammed 'DIMWA', alisema utekelezaji wa ilani katika mkoa wa Kaskazini imekuwa ikitekelezwa kwa vitendo ikiwemo ujenzi wa shule mpya tano za ghorofa.

Alisema ndani ya miaka miwili ya dk.mwinyi maendeleo yamefikiwa kwa kiasi kikubwa na kumtaka makamu kuendelea kuwatumikia wananchi na kutokuvunjika moyo katika utekelezaji wake wa ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Pia,alisema CCM itaendelea kuisimamia serikali ili kuona maendeleo yanawafika wananchi ikiwemo kusimamia miradi inayotekelezwa na kuhakikisha kauli zinakuwa moja kati ya serikali na Chama.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi