RAIS DK HUSSEN ALI MWINYI AMESEMA SERIKALI ZOTE MBILI ZITAENDELEA KUTEKELEZA KIKAMILIFU DIRA NA MIPANGONYA MAENDELEO, ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2020-2025, PAMOJA NA SERA NA MIKAKATI YA MAENDELEO ENDELEVU YA SEKTA YA UVUVI NCHINI.
Ameyasema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika sherehe ya siku ya Uvuvi Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.
Rais Dkt Mwinyi amesema katika kukuza na kuimarisha minyororo ya thamani ya Sekta ya Uvuvi na Mazao ya Baharini, Serikali itaendelea kupiga vita Uvuvi haramu na kuvitaka vyombo husika kuendelea kuchukua hatua zinazostahiki katika kupiga vita Uvuvi haramu.
Amesema kuwa uwepo wa siku ya Uvuvi Duniani inatokana na Tamko la Umoja wa Mataifa la kushajihisha Uvuvi endelevu wenye tija kwa wananchi hivyo Serikali zitaendelea kuwawezesha wavuvi kwa kuwapatia elimu, nyenzo, mitaji na masoko ili kuweza kujipatia ajira na kipato kinachokidhi mahitaji.
Aidha Rais Dkt Mwinyi amesema serikali itaendelea kuwapatia vyombo na nyenzo za kisasa zitakazowawezesha kuingia katika Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na kuwawekea miundombinu iliyo bora ikiwemo ujenzi wa madiko ya kisasa, masoko na mitambo ya kuhifadhia samaki.
Sambamba na hayo Dkt Mwinyi amesema katika kuhakikisha sekta ya Uvuvi inafanikiwa zaidi Serikali zimejipanga kujenga viwanda vya kusarifia na kuchakata minofu ya samaki na dagaa pamoja na kuwekeza zaidi kwa kuwawezesha wavuvi kufuga na kuzalisha samaki katika bahari na maji baridi.
Amesema kuwa kupitia programu ya Ahuweni ya UVIKO 19 ya Uchumi wa Buluu kwa Zanzibar jumla ya Boti 577 za uvuvi zimetolewa, Boti 500 wamepatiwa wakulima wa mwani, vifaa vya uvuvi kama vile mishipi, nyavu, GPS na fish finders, kamba na tai tai kwa wakulima wa mwani pamoja na kujengwa kiwanda cha kisasa cha kusarifia Mwani.
Kwa upande wake waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Abdalla Khamis Olega amesema wizara zote mbili zitahakikisha zinatoa fursa sawa kwa wavuvi wa pande zote mbili kwa kuwapatia vitendea kazi ili kuwaweza kuvua kisasa.
Amesema kwa Tanzania bara zaidi ya wavuvi laki moja na tisiini na saba tayari wameshapatiwa leseni za Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na kupatiwaa zana zote ambazo zitawasaidia kuvua kisasa sambamba na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Nae Mkurugenzi Mkaazi kutoka shirika la Chakula Duniani (WFP) BIbi Sara Golden Gipson amesema WFP imekuwa ikichangia katika shuhuli za maendeo ya Uchumi wa Zanzibar hasa katika Sekta ya Uvuvi sambamba na kuwanyanyua wanawake kiuchumi kwa kuwajengea uwezo pamoja na kuwapatia miradi mbali mbali ya kimaendeleo.
Sara amesema WFP imekuwa ikiwasaidia wanawake katika kuhakikisha wanapiga hatua za maendeleo kwa kuwatatulia changamoto mbali mbali zinazowakabili katika shuhuli zao kama vile uhaba wa vitendea kazi hasa kwa wakulima wa mwani pamoja na kuwapatia maboksi ya kuhifadhia samaki kwa muda refu.
Mwakilishi huyo wa WFP ameishukuru Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaamini na kuwapatia mashirikiano katika kazi zao sambamba na kuahidi kuendelea kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanziabar kwa kasi zaidi ili kuhakikisha malengo mkakati ya Serikali kupitia Uchumi wa Buluu yanafikiwa.
Katika sherere hiyo Mhe. Hemed alizindua vitabu mbali mbali kwa niaba ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ikiwa ni pamoja na Sera ya Uchumi wa Buluu Zanzibar, Mkakati wa Uchumi wa Buuu Zanzibar, Sera ya Uvuvi Zanzibar, Mkakati wa Uvuvi Zanzibar, Mpango Mkuu wa Uvuvi Zanzibar pamoja na Mpango kazi wa Ukondoishaji wa masuala ya Kijinsia katika Uchumi wa Buluu.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekagua mabanda ya maonesho ya shuhuli mbali mbali zinazofanywa na Wizara, Taasisi Binafsi na wadau wa Uvuvi katika sherehe ya siku ya Uvuvi Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
26-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
26-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
26-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
26-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
26-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
26-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
26-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
26-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
26-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
26-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
26-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
26-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
26-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
26-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
26-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
26-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
26-05-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
26-05-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
26-05-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
26-05-2026