Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEAHIDI KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHI NZIMA.

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa ahadi hiyo Ikulu, Zanzibar alipojumuika kwenye chakula cha mchana na wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15, Karume Boys, baada ya kunyakua kombe la CECAFA nchini Uganda.

Dk. Mwinyi alisema michezo ni afya, ajira, utalii pia huwaunganisha jamii kwa watu kufurahi pamoja na kuwa kitu kimoja. Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema Zanzibar haitegemei utalii wa urithi pekee unaotokana na hifadhi ya Mji Mkongwe pamoja na fukwe lakini pia michezo ni utalii mkubwa na wakutegemewa.

Alisema Zanzibar inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano ya AFCON mwaka 2027 hivyo imejipanga kuimarisha miundombinu ya kisasa kwenye sekta ya michezo pamoja na kushajihisha sekta ya utalii hususani hoteli na nyumba za kufikia wageni.

Naye Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita alisema Wizara ilipewa dhamana na Serikali ya kuisafirisha timu hiyo ambapo Rais Dk. Mwinyi alitoa usafiri wa ndege kwa Karume Boys kama zawadi wakati wa kurejea nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Muhamed Said Dimwa alishauri kupatiwa mafunzo maalumu ya michezo walimu wawili kwa Karume Boys. Kwa upande wake Rais wa ZFA, Suleiman Mahmoud Jabir alisema mafanikio ya ushindi wa Karume Boys yaliyokana na juhudi na ushirikiano wa wadau wengi nchini.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi