Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar , imeridhishwa na hatua nzuri ya ujenzi wa skuli za Sekondari za ghorofa ( G+3 ) zinazojengwa na Kampuni ya Simba Developers Ltd  katika kijiji cha Bumbwini Makoba na Bumbwini Misufini Wilaya ya Kaskazini “ B”  Unguja.

alternative

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa skuli hizo pamoja na kumbi za Mitihani zinazojengwa katika skuli hizo, Mhe.Hemed amesema wakadarasi kutoka kampuni ya Simba Developers wanaendelea kuipatia heshima kampuni yao sambamba na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya nane ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

 

 Amesema kuwa Serikali imekusudia kuondoa changamoto zote zinazowakabili wananchi wa mijini na vijijini ikiwemo chanagamoto ya msongamano wa wanfunzi madarasani na kuingia kwa mikondo miwili ya masomo hivyo ameitaka kampuni ya Simba Developers inayojenga Skuli hizo  kuongeza kasi zaidi ili kuweze kumalizika kwa wakati ujenzi huo,

 

Aidha Mhe. Hemed ameitaka Wizara ya Elimu kukaa pamoja na viongozi wa Jimbo la Bumbwini kuangalia namna watakavyoifanyia ukarabati skuli ya Msingi ya Bumbwini Makoba na kuliangalia kwa umakini suala zima la ajira hasa katika kuajiri walimu wazawa ambao watasaidia kuondosha changamoto ya walimu kuchelewa kufika maskulini na kuzorotesha maendeleo katika Sekta ya Elimu.

 

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais amesema Serikalini ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuzisimamia changamoto zote na kuzitafuta ufumbuzi na kuwaahidi wananchi wa Bumbwini waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo kuwa Serikali itahakikisha inawapatia stahiki zao kwa mujibu wa taratibu na sheria.

 

Aidha Mhe. Hemed amewataka Wananchi wa Bubwini  na wazanzibari kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Hussen Mwinyi pamoja na Serikali zote mbili katika jitihada wanazozifanya za kuwaletea maendeleo na kuwataka kukipa mashirikiano chama cha Mapinduzi ili kiendele kushikilia dola katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020-2025, Sambamba na kuwasisitiza kuendelea kuitunza na kuidumisha amani iliyopo nchini kwani hakuna Taifa lolote litakalopiga hatua za kimaendeleo bila ya kuwa na Amani, Umoja na mshikamano.

 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulghulam Hussein amesema Mipango ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ni kuhakikisha ifikapo Januari 2025 wanafunzi wote wa Zanzibar wawe wanaingia skuli kwa mkondo mmoja wa asubuhi pamoja na kuondoa changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani.

 

Aidha Mhe. Ghulam amesisitiza kuwa vifaa vyote kwa ajili ya skuli mpya zinazojengwa na zinazofanyiwa ukarabati vipo tayari na hakuna skuli itakayokosa vifaa vya kufundishia na kusomea kwa wanafunzi wote wa Zanzibar.

 

Mhe. Ghulam amesema  Serikali imeongeza Bajeti ya Wizara ya Elimu na kufikia zaidi ya Bilioni 800 kwa mwaka wa fedha 2024-2025 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kujengea skuli za ghorofa za kisasa, kuzifanyia ukarabati skuli ambazo ni chakavu na kujenga madarasa mapya kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.

 

Kwa upande wake mkandarasi anaenjenga skuli hizo pamoja na kumbi za Mitihani Simba Developers Ltd amesema wapo katika hatua za mwisho za ujenzi na kuahidi kuwa mwishoni mwa mwezi wa saba wanatarajia kuzikabidhi skuli hizo Serikalini ili wanafunzi waweze kuendeleo na masomo yao katika skuli hizo.

 

Kampuni ya Simba Developers wamemshukuru Rais Dkt Mwinyi kwa kuwaamini na kuwapatia nafasi ya kujenga miradi mbali mbali ya amendeleo hapa Zanzibar na kuahidi kuwa watahakikisha wanajenga kwa ubora na kwa viwango vinavyokubalika ili majengo hayo yaweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu pasipo na changamoto za aina yoyote za kiufundi.

 

Katika ziara hio Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ametembelea ujenzi wa skuli ya Ghorofa ya Bumbwini Makoba, na Bumbwini Misufini na kumbi za Mikubtano . katika skuli hizo ,

alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi