MAKAMU WA PILI ZANZIBAR MHE. HEMED SULEIMAN AZINDUA BARAZA LA MANISPAA LA CHAKE CHAKE PEMBA
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka uongozi wa Baraza la Mji la Chake Chake Pemba ambalo limepandishwa hadhi na kuwa Baraza la Manispaa Chake Chake kuhakikisha wanasimamia vyema vyanzo na ukusanyaji mzuri wa mapato ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.Ameyasema hayo wakati akizindua Baraza la Manispaa Chake Chake Pemba katika Viwanja vya Tibirinzi Pemba Mhe. Hemed ameipongeza Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kasi kubwa ya kuimarisha utendaji kazi katika Serikali za Mitaa na kuridhia mapendekezo ya kulipandisha hadhi Baraza la Mji Chake Chake na kuwa Baraza la Manispaa Chake Chake Pemba kwa kuzingatia Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Amesema kuwa matarajio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Baraza hilo jipya litahakikisha huduma za kijamii zinakuwa bora na za ufanisi zaidi ambazo zitawaondolea usumbufu wananchi kwa kupata huduma hizo pamoja na kuandaa mipango bora ya kimkakati itakayotoa tija kwa Wananchi na Serikali kwa ujumla.
Aidha Mhe. Hemed amewasisitiza Watendaji wa Baraza la Manispaa Chake Chake kusimamia vyema makusanyo kwa kutumia mifumo ya risiti za kielektroniki, kuwa na matumizi sahihi ya rasilimali watu na rasilimali fedha, kuibua Miradi mbali mbali ya maendeleo, kuimrisha usafi wa mazingira na kusimamia Amani na mshikamano katika jamii.
Amelitaka Baraza la Manispaa Chake Chake Pemba na watendaji wake kukemea vitendo vya rushwa na utumiaji mzuri wa rasilimali za Serikali, kuacha ,uhali na kutanguliza maslahi ya Taifa ili kuwa Baraza la mfano litakalotoa hamasa wa ushindani wa kimaendeleo kwa kuongeza mapato Serikalini na kuzitumia fursa mbali mbali zinazopatikana katika Wilaya hiyo.
Ameutaka Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba kuwa na mipango shirikishi jamii kwa kuzishirikisha Kamati za mashauriano za Shehia na Mabaraza ya wadi, Kamati za Wilaya na Mikoa ili kupata mazingatio na ushauri katika maendeleo.
Sambamba hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefahamisha kuwa endapo Mabaraza ya Manispaa na Miji Zanzibar yatatekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Serikali za Mitaa yataleta matokeo mazuri yenye tija na kuepusha Migogoro katika jamii.
Pamoja na hayo amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuridhia Baraza la Mji la Chake Chake Chake kupandishwa hadhi na kuwa Baraza la Manispaa kumetokana na miongozo na maelekezo yake kwa watendaji wa Baraza hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed ameishukuru Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuridhia kulipandisha hadhi Baraza la Manispaa Chake Chake ni kurahisisha kasi ya upatikanaji wa maendeleo na ukuwaji wa uchumi ndani ya Mkoa huo.
Aidha amewataka watendaji wa Baraza la Manispaa Chake Chake kwa kushirikiana na wananchi kuongeza kasi katika utendaji wao wa kazi, kuwa wabunifu wa miradi mbali mbali itakayowaongezea kipato kitakachosaidia kukuza uchumi hasa katika Mkoa huo.
Amesema mashirikiano ndio silaha katika kutimiza majukumu yetu ya kazi na kuwataka kuachana na kufanya kazi kwa utashi binafsi na kuelekeza nguvu zao katika kulitumikia Taifa.
Sambamba na hayo Mhe. Masoud amemuhakikisha makamu wa pili wa rais wa Zanzibar wizara itahakikisha inafata maelekezo na maagizo yote yanayotolewa na viongozi wakuu wa nchi katika kuwaleetea maendeleo wananchi wote pamoja na kuifata ilani ya chama cha mapinduzi ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mattar Zahor Massoud amesema endapo viongozi watafanya kazi kwa pamoja hasa katika shuhuli za maendeleo na kuwataka kuachana na tabia ya kukwamisha na kuzorotesha Miradi mbali mbali ya maendeleo kwani kufanya hivyo ni kuikwamisha Serikali kwa ujumla.
Mhe. Mattar ameahidi kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na viongozi na wananchi kwa kufuata miongozo ya Nchi na kamwe hatokatishwa tamaa na wachache wasioitakia mema nchi yetu na amesema jitihada pekee ndio zitakazolipandisha zaidi Baraza hilo la Manispaa kuwa Jiji muda mfupi ujao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa chake chake Ndugu Maulid Mwalim Ali amesema kupandisha hadhi kwa baraza la manispaa la chake chake kutawajengea ari na morali wafanyakazi katika kufanya kazi kwa umakini na weledi wa hali ya juuu katika kufanikisha malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Amesema Baraza la Manispaa Chake Chake litahakikisha linaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kuimarisha usafi wa mazingira na kuendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo pamoja na kuwapatia elimu zaidi wafanyakazi ili kuleta ufanisi nzuri wa kazi.
Aidha amesema Baraza la Manispaa Chake chake litafanyakazi kwa kasi na ufanisi zaidi ili kuhakikisha linapanda hadhi Zaidi kwa maslahi ya wanachi na Taifa kwa ujumla
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
30-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
30-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
30-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
30-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
30-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
30-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
30-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
30-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
30-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
30-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
30-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
30-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
30-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
30-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
30-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
30-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
30-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
30-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
30-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
30-05-2026