RAIS SAMIA AMEAMUA KUIFUNGUA MIKOA YA KUSINI KIUCHUMI
Ni barabara ya uchumi Mtwara- Tandahimba- Newala- masasi( 210Km)
MTWARA: Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuifungua mikoa ya Kusini kiuchumi kwa kutenga kiasi cha Sh bilioni 234 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kiuchumi yenye umbali wa kilometa 210.
Makalla alieleza hayo leo Aprili 15,2025 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 10 mkoa wa Lindi na Mtwara.
Aidha, Makalla amesema kuwa Rais Samia amemtuma apite kukagua barabara hiyo ambayo imetajwa kuwa ya kiuchumi na kueleza kuwa hadi sasa kilometa 50 tayari zimekamilika na alijiridhisha kuwa ujenzi bado unaendelea kufanyika kwani amewakuta wakandarasi wakiendelea na maandalizi ya kuikamilisha.
Makalla amesema kuwa Rais Samia anania njema na wananchi wa Kusini mwa Tanzania na katika kutaka kuiimarisha mikoa hiyo kiuchumi ametenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo itakayosaidia katika kuendeleza uchumi.
Akifafanua sababu za barabara hiyo kuwa ya kiuchumi Makalla alisema Rais Samia amefungua mikoa hiyo akiwa na lengo la kuiboresha iweze kukua kwa kuanza na kutoa kiasi cha Sh bilioni 157 kwa ajili kuboresha na kupanua bandari ya Mtwara ambayo itasaidia na kurahisisha usafirishaji wa Korosho kutoka Mtwara kwenda katika maeneo mengine.
Pia amesema kuwa hapo awali Rais Samia alifika Mtwara na kuweka jiwe la msingi katika barabara hiyo inayotoka Newala, Tandahimba hadi Masasi ambayo inakwenda kuunganisha Mtwara na maeneo mengine ya Mchuchuma na Mbamba Bay ambayo.
“Rais Samia amenituma, Mwenezi ukienda huko ukague na hiyo barabara ya kilometa 210, kilometa 50 zipo tayari angalia kama ujenzi unaendelea nimethibitisha nimempita mkandarasi maandalizi yanafanyika vipande viwili kilometa 100 amepewa mkandarasi mmoja, kilometa 60 kapewa mwingine zote 210 mpaka Masasi zinajengwa,” amesema Makalla.
Ameongeza kuwa ili bandari iweze kufanya kazi vizuri na kuleta tija ni baada ya kukamilika kwa barabara hiyo ambayo kusaidia kuimarika kwa uchumi katika mikoa yote ya kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma itakuwa imefunguka vizuri.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
25-10-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
25-10-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
25-10-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
25-10-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
25-10-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
25-10-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
25-10-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
25-10-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
25-10-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
25-10-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
25-10-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
25-10-2025
TAARIFA KWA UMMA
25-10-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
25-10-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
25-10-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
25-10-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
25-10-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
25-10-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
25-10-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
25-10-2025