Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
WANA CCM WAMERIDHIA DKT. SAMIA KUONGEZEWA MIAKA 5 KUONGOZA TAIFA LETU - BALOZI DKT. NCHIMBI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi , amesema katika ziara yake ya siku 10 hadi kufikia sasa ametembelea mikoa sita na Nyanda za juu kusini ambapo kote alipopita amethibitishiwa na wanachama wa CCM kuwa wanataka Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, apewe miaka mitano mingine ya kuliongoza Taifa kutokana na kile wanachoendelea kukiona cha kufanyika kwa kazi kubwa na nzuri kila kona ya Nchi katika kuleta maendeleo kwa nchi na wanachi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano ulioshirikisha Mabalozi wa mashina, viongozi mbalimbali wa chama na serikali, viongozi wa dini, taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali, wazee, machifu na wadau mbalimbali wa maendeleo, Balozi Dkt. Nchimbi amesema wanachoanua wanachama wa CCM ndicho kitakachotokelezwa kwasababu hakuna enek la nchi ambalo halijaguswa kimaendeleo na ndiyo sababu ya wababchama kufikia uamizi huo.
" Sehemu zote tulizopita na viongozi wenzangu ujumbe tuliyoupata ni Viongozi na wana CCM kwa ujumla wamesema Mama Samia ni mitano tena na mimi ndiye ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ndani ya chama sasa mimi nani hadi niwakatalie wanachama...wanachoanua wana CCM ndicho tunachotekeleza "
" Wana CCM wanataka kuona Rais Dkt. Samia anapewa miaka mitanao na agizo hio linatokana na kazi nzuri ambayo Rais Samia ameifanya, hakuna sehemu ya nchi ambayo haijaguswa kwa maendeleo, tuendelee kumuunga mkono Rais wetu na kueleza kwa watu wote kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwakuwa inaonekana ila wapo baadhi ya watu watajifanya kama hawaoni "
Alisema Balozi Dkt. Nchimbi.
Aidha, Dkt. Nchimbi ametoa wito kwa wanachama wa CCM wa kuwatala kuendeleza umoja na mshimano kwasababu chama kina wajibu wa kuwatumikia Watanzania.
"Tukiwa na mshikamano nchi itashikamana, kama tukiwa na mafarakano na nchi itafarakana. Kila mwana CCM ajiulize anatoa mchango gani katika nchi yake ?"
"Kila mwana CCM ajiepushe kuwa chatu mbaya ndani ya chama na tujiepushe kwa kutimiza wajibu wetu. CCM lazima iendeee kuwa kimbiio la Watanzania."
"Kiongozi wa kweli hamdharau Mtanzania mwenzake bali ana wajibu wa kumpenda kila mtu, Chama hiki siyo viongozi ni chama cha wananchi"
Alisema Balozi Dkt. Nchimbi.
🗓️22 Aprili, 2024
📍Mbinga - Ruvuma
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.