Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


WASIRA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MBOZI WILAYANI MBOZI

alternative

 

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amekagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Wasira alikagua miradi hiyo leo Machi 15, 2025 ambapo moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Songwe iliyopo Vwawa wilayani Mbozi, ambapo serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa sh. bilioni 16 kufanikisha ujenzi wake.

Pia, Makamu Mwenyekiti Wasira alipata fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Hiloli ambapo alizungumza na wanafunzi wa darasa la saba wanaojiandaa kufanya mtihani wa taifa mwaka huu.

Aliwahakikishia wanafunzi hao kuwa serikali chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia itaendelea kuwajengea mazingira mazuri kuhakikisha wanapata elimu bora kuanzia msingi hadi chuo kikuu.
 

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine