WAKASUVI AMEFIKWA MAUTI KATIKATI YA JUKUMU ZITO: DKT. NCHIMBI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Hassan Mohamed Wakasuvi ni pigo kubwa, si kwa mkoa huo pekee, bali Chama, Serikali na taifa zima kwa ujumla, ambapo amefikwa na mauti akiwa ni Mwenyekiti wa Kamati Ndogo, iliyopewa jukumu la kuangalia namna ya kukiboresha Chama Cha Mapinduzi.
Dkt. Nchimbi amesema kuwa Komredi Wakasuvi alikuwa mmoja wa viongozi shupavu wa Chama Cha Mapinduzi, kuanzia mkoani kwake, hadi ngazi ya taifa, ambapo kutokana na uwezo na uadilifu wake katika kutimiza majukumu yake kwa ufanisi na ushirikiano tangu alipochanguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, mwaka 2007, aliendelea kuaminiwa hadi kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, nafasi aliyokuwa nayo hadi mauti yalipomfika.
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akitoa salaam za pole na rambirambi kwenye msiba wa Mzee Wakasuvi, kabla ya mazishi ya kiongozi huyo, Jumamosi Februari 24, 2024, katika Kijiji cha Mabama, Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, uliohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Kiwango cha kuaminiwa Mzee Wakasuvi kilikuwa ni kikubwa sana. Mbali ya kuwa Mwenyekiti wa Mkoa na Mjumbe wa NEC ya CCM Taifa, pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu. Lakini pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati iliyopewa jukumu la kuangalia namna ya kukiboresha Chama chetu. Makamu wake alikuwa ni Mzee Wassira (Steven).
“Wanauliza watu maswali mbalimbali. Mimi ilikuwa imepangwa niwatembelee na kuonana nao Jumatatu (keshokutwa). Wakaniulize maswali waliyopanga kuniuliza nami nilikuwa nimejiandaa kwenda kujibu maswali hayo,” amesema Dkt. Nchimbi na kuongeza;
“Ameanza uongozi muda mrefu sana tangu Umoja wa Vijana. Wenzake wengine wako hapa akina Mzee Lukuvi (William), Mzee Luhavi (Rajabu) na wengine. Muda wote alikuwa anahamasisha maendeleo ya nchi yetu na kuchochea uimara wa CCM. Chama kimepoteza, Serikali imepoteza na Wananchi kwa ujumla wamepoteza kiongozi mahiri na shupavu. Tuna kila sababu ya kulinda na kuenzi kazi zake, kwa kuendelea kuwa na umoja, kushikamana, amani na utulivu thabiti bila kujali tofauti zetu za kisiasa, dini, kabila wala maeneo.”
Mbali ya salaam hizo, Dkt. Nchimbi pia aliwasilisha salaam za Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo Katibu Mkuu wa CCM huyo amesema kuwa msiba huo umemgusa Mheshimiwa Rais moja kwa moja lakini hakuweza kuhuduria kutokana na ratiba ya majukumu mengine ya kikazi, nje ya nchi.
“Kama ambavyo imekuwa kawaida kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kila kunapojitokeza jambo kama hili, hapa pia amejitoa kwa uzito mkubwa tangu tu zilipotokea taarifa za msiba huu. Washauri wake wa siasa wote wako hapa. Pia ametutuma sisi wasaidizi wake, Mhe. Waziri Mkuu kwa upande wa Serikali na mimi kwa upande wa Chama kuleta salaam zake za pole kwa wanaCCM wote na Tabora kwa ujumla wenu. Nasi pia tutafikisha salaam na shukrani zenu mlizompatia yeye kwa jinsi alivyojitoa kushiriki katika msiba huu,” amesema Dkt. Nchimbi.
Mzee Hassan Mohamed Wakasuvi alifikwa na mauti siku ya Alhamis, Februari 22, 2024, baada ya kuugua kwa muda mfupi, ambapo pia alikuwa katika maandalizi ya kusafiri kikazi kwenda mkoani Pwani, Jumapili, Februari 25, 2024 kwa ratiba ya majukumu mengine ya kazi za Chama.
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
26-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
26-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
26-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
26-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
26-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
26-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
26-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
26-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
26-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
26-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
26-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
26-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
26-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
26-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
26-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
26-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
26-05-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
26-05-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
26-05-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
26-05-2026