Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya CPC Jimbo la Shanxi, Komredi Tang Dengjie.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya H/kuu ya CCM Taifa Mhe. Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya CPC Jimbo la Shanxi, Komredi Tang Dengjie. Katika kikao hicho kilichofanyika Juni 21, 2024, katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni, Dar es Salaam, Chama Cha Mapinduzi kiliwakilishwa na Katibu wa NEC, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Rabia Abdalla Hamid.
Katika mazungumzo hayo, Ndg. Majaliwa alisisitiza kuendelea kudumishwa kwa ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na China.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.