Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
NAFASI KUBWA KULIKO ZOTE KWENYE CCM NI UANACHAMA - DKT. NCHIMBI
> Apiga marufuku kuendeleza makundi baada ya chaguzi za ndani
> Awataka viongozi kutambua nafasi zao za utumishi
"Niwasihi wana CCM kataeni viongozi wa kuandikiwa, wa kuletwa mfukoni ninyi mnaishi na watu kwenye maeneo yenu na mnawajua , chagueni watu kwa sifa na mtu apewe kwa sifa zake sio za rafiki au mpambe wake"
"...lakini tujue kwenye uchaguzi kuna kusinda na kushindwa hivyo ni lazima tukubali matokeo mara baada ya chaguzi"
"Makosa makubwa ni kuendeleza makundi ya uchaguzi baada ya uchaguzi , makundi yaishe mara tu baada ya uchaguzi kutangazwa"
"Nafasi kubwa kulikonzote ndani ya CCM ni UANACHAMA, usichaguliwe kuwa kiongozi ukajiona wewe ndio mkubwa kuliko wote, wewe ni mtumishi na mda wowote unaweza kutumika sehemu nyingine kwa maslahi ya watu wote na sio kutumia nafasi yak kwa kuweka makundi"
"Viongozi lazima watambue nafasi zao za utumishi, ukiwa Mbunge unajua wewe ni mtumishi wa wananchi wako, ukiwa Waziri utambue wewe ni mtumisi wa wananchi wako ukitaka kujifanya boss lazima utapata changamoto kwenye uendeshaji wa eneo lako"
Vile vile, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameonesha hali ya kusikitishwa na suala la mmomonyoko wa maadili uliyokithiri Nchini.
Balozi Dkt. Nchimbi amekemea vikali tabia hiyo kwa baadhi ya wazazi na walezi wanoshindwa kutimiza wajibu wao vizuri na kupelekea watoto na vijana wengi kuwa na tabia zisizofaa katika jamii.
Akizungumza kwenye mkutano uliokutanisha Mabalozi wa mashina wa CCM , Viongozi wa Serikali, Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali , Wazee na Viongozi wa Dini, Dkt. Nchimbi amewataka kwa pamoja kuwa sehemu ya kuendelea kuwa walinzi wazuri kwa watoto na vijana.
Dkt. Nchimbi ametoa shukrani za CCM kwa Viongozi wa Dini kwa kuendelea kuliombea Taifa kuendelea kuwa na Amani na Utulivu wakati wote.
" Viongozi wa dini mnafanya kazi kubwa sana katika kuuiombea na kuilinda Amani na Mshikamano wa Nchi yetu "
" Kuna wakati mnasali na kutufanya hadi anayesikiliza maombi kujiona na kutambia kwamba unayo sababu ya kuilinda Amani ya Nchi yetu "
" Nawaomba viongozi wa dini endeleeni kutoa maombi ya kuliombea Taifa katika masuala ya mmomonyoko wa maadili, kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa vijana na watoto wetu "
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Katibu Mkuu wa CCM
Akizungumza na Mabalozi wa mashina, Viongozi mbalimbali wa serikali, Taasisi zisizo za kiserikali, Wazee na Viongozi wa Dini.
📍Sumbawanga - Rukwa
🗓️ 15 Aprili, 2024
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.