Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Wanachama wa CCM na Wazanzibari kwa ujumla wana kila sababu ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi kwa mafanikio na maendeleo makubwa aliyoiletea Zanzibar.

alternative

Ameyasema hayo katika Hafla Maalum ya Usiku wa Kumpongeza Mhe.Dkt Hussein Mwinyi kwa kutimiza Miaka minne ya mafanikio katika uongozi wake iliyofanyika katika Kiwanja cha kufurahishia watoto TIBIRINZI CHAKE CHAKE PEMBA, iliyoaandaliwa na Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Amesema katika Uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi maendeleo ya wazi yanaonekana kila kona na hakuna eneo ambalo Dkt. Mwinyi hajalifikia kimaendeleo  ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais ambae pia ni Mjume wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa amewataka Wazanzibari kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Mwinyi pamoja na Serikali anayoiongoza ili kumpa nguvu zaidi ya kuendelea kuwatumikia Wazanzibari kwa mafanikio makubwa zaidi.

Aidha, Mhe. Hemed amesema Rais Dkt Mwinyi ni msikivu na mwenye kupenda umoja na mshikamano kwa wanachi wake hivyo Serikali anayoiongoza ipo tayari kupokea ushauri wenye tija utakaoileta Zanzibar maendeleo kwa maslahi mapana ya wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Sambamba na Hayo amesema Mwaka wa tano (5) wa uongozi wa Dkt Mwinyi utekelezaji wake wa maendeleo utakuwa wa kupigiwa mfano ambapo miradi mingi na  mikubwa ya maendeleo itakatekelezwa kwa  lengo la kuendelea kunyanyua uchumi wa  wazanzibari.

Nae  Katibu wa Idara ya Siasa, Itikadi, Uwenezi na Mafunzo ya CCM Zanzibar Komredi KHAMIS MBETO amesema Chama cha Mapinduzi kina kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt Mwinyi kwa mema na mazuri anayoendelea kuwafanyia wananchi wa Zanzibar.

Komred MBETO amesema wana CCM na wananchi wa Zanzibar wataendelea kumuunga mkono Dkt Mwinyi kwa dhamira yake njema ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari wote pasipo kujali rangi, kabila, dini wala jinsia zao.

 

alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi