Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


SONGWE NI IMARA SABABU VIONGOZI WOTE WANAONGEA LUGHA MOJA - MWENEZI MAKALLA

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM , Itikadi, Uenezi na Mafuzo Ndugu. Amos Makalla , amesema lengo la Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Nchimbi ni kuona na kutambua katika mambo makubwa manne ambayo ni kuona uhai wa chama (CCM) ,maandalizi ya uchaguzi, kuona utekelezaji wa ilani ya CCM na kupata kero na changamoto.

Akizungumza katika mkutano ulikutanisha Viongozi na Wajumbe mbalimbali wa CCM, Vingozi wa serikali, Taasisi zisizo za kiserikali, Wazee, Machifu na Viongozi wa dini, Mwenezi Makalla amesema "...sisi katika ziara yetu tunataka kukipa chama chetu heshima yake, utaratibu wa CCM ukiandaa ziara lazima ufike katika ofisi ya chama na upokee taarifa zote za utendaji wa kazi ya chama na utekelezaji ilani wa serikali"

"Taarifa zote tulizopokea na kujionea zimedhiirisha Mama Samia amepiga kazi kubwa sana na hapa mkoani Songwe hakuna haja ya kuita huu mkoa kitinda mimba sababu miradi ya maendeleo ni mingi na imetekelezwa, awamu ya sita hii mmepewa fedha nyingi kuliko awamu zote na utulivu wa kisiasa umekuwa wa hali ya juu na hii ni sababu mmeweka wabunge wazuri wa CCM kwakuwa wataongea lugha moja na serikali inayotokana na CCM."

"Mafanikio yaliyopatikana tuendelee kuyasimamia na siri yake ni umoja na mshikamano, endeleeni kuunga mkono Chama Cha Mapinduzi."

"Tuendelee kutambua kuwa kjikosoa ni silaha ya Mapinduzi."

Pia, Mwenezi Makalla amesema amewataka Viongozi wote wa Chama na Serikali kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.

"Wana CCM msiogope kusema mafanikio tuliyopata hadi sasa kutokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dkt. Samia katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini"

"Serikali imekuwa ikikusanya fedha nyingi na kuzitumia katika shughuli za kimaendeleo ...ndio maana hata hapa mkoani Songwe tunaona namna kazi kubwa inafanyika"

"...CCM inawataka viogozi wote wa serikali kufanya kazi ya kusikiliza na kutatua kero msisubiri hadi viongozi wa kitaifa, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya fika kwenye eneo lako sikiliza na tatua , lakini jambo ili liende sambamba na viongozi wa CCM kwakuwa ni wajibu wetu kwasababu serikali iliyopo madarakani inatokana na Chama Cha Mapinduzi"

"Bebeni kero za watu, fungueni milango wasikilizeni, jengeni imani hiyo kwa wananchi ya kwamba CCM ndicho chama kilichopewa dhamana."

🗓️16 Aprili, 2024
📍Mbozi - Songwe

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi