MJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NDUGU HEMED SULEIMAN ABDULLA AMESEMA CHAMA CHA MAPINDUZI KITAENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM KWA KUIJENGA ZANZIBAR YA KIUCHUMI KWA KUTATUA NA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KIVITENDO.
Akizungumza na wana CCM na wananchi wa Jimbo la Magomeni na Jimbo la Kikwajuni amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kushinda na kushikilia Dola kwa Vile Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ana dhamira na nia thabiti ya kuwaletea Wazanzibari maendeleo endelevu.
Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa nguzo pekee ya kukijenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi ni umoja na mshikamano ndani ya chama kwa viongozi kushirikiana katika kuwatumikia wanachama na wananchi wote kwa haki na usawa, ukweli na uwazi katika kukijenga Chama.
Amesema kumekuwa na makundi ya wapambe katika Chama yanayobeba Viongozi na wagombea ambapo ni vyema kuungana na kuacha kujenga mgawanyiko katika CCM na watumie ujuzi na nguvu zao katika kuunganisha wanachama kukiendeleza Chama Cha Mapinduzi.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, amewataka Viongozi wa ngazi mbali mabali katika chama kujitahidi katika kusajili wanachama wapya, kusimamia wanachama waweze kulipa ada kwa wakati na kupatiwa kadi za kieletroniki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Ndugu Talib Ali ameeleza kuwa kumekuwa na viongozi wa vyama vya upinzani wanapotosha umma wa wazanzibari kwa kuichafua Serikali ya Dkt. Mwinyi na kuwasihi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kueleza mazuri yanayofanywa na Viongozi wetu wanaopenda maendeleo.
Amesema ikiwa wanachama wa CCM na wazanzibari wataungana pamoja hatutokuwa na mwanya kwa wasopenda maendeleo kuisema vibaya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe. Rashid Simai Msaraka ameeleza kuwa Ziara ya hiyo ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni ya mafanikio ambapo inadhihirisha utayari wa viongozi wakuu wa Serikali katika kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.
Mhe. Msaraka ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mjini ameeleza kuwa kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 tayari utekelezaji wa Ilani hiyo umekamilika kwa asilimia Mia Moja (100) kwa kuzingatia sekta mbali mbali ikiwemo Michezo, Elimu, maji na miundombinu ya Barabara.
Kwa upande Viongozi wa Majimbo hayo wamemshukuru na kumpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kutembelea Majimboni na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwani ujio huo unatilia mkazo na kuwakumbusha majukumu yao.
Wamemuhakikishia kuwa ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi ni wa lazima katika majimbo hayo kwani wanachama wa CCM wameridhika na utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa maendeleo yanayoletwa na Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi .
Katika ziara hiyo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ameweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Tawi la CCM Nyerere 'A' pamoja na kukabidhi hati ya Nyumba iliyonunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la CCM Meya Bondeni ambapo ameupongeza Uongozi wa Jimbo la Magomeni kwa kuona umuhimu wa kuwa na majengo ya kisasa na ya kutosha kwa ajili ya watendaji wa Chama Cha Mapinduzi.
Amesema ujenzi wa Ofisi hizo unadhihirisha juhudi za Viongozi wa Jimbo hilo kuunga mkono maelekezo ya Viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi kuwawekea mazingira mazuri watendaji ili wafanye kazi katika mazingira mazuri.
Aidha Mhe. Hemed ametembelea mradi wa maji Kikwajuni Mzimni ambao umesita kwa muda mrefu na kueleza kuwa Serikali itatafuta wataalamu kuangalia namna bora ya kukamilisha mradi huo ili uwafae wananchi wa maeneo hayo.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
28-10-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
28-10-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
28-10-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
28-10-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
28-10-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
28-10-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
28-10-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
28-10-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
28-10-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
28-10-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
28-10-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
28-10-2025
TAARIFA KWA UMMA
28-10-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
28-10-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
28-10-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
28-10-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
28-10-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
28-10-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
28-10-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
28-10-2025