Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
SERIKALI YA RAIS SAMIA IMETENGA BILIONI 227.9 KWA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU
> Asema hii ni fursa katika kujiendeleza kiuchumi
> Atoa maagizo kwa UVCCM na UWT kuhamasisha juu ya mikopo ya 10% kutoka Halmashauri
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu. Amos Makalla amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, imerejesha mikopo ya asilimia 10% ya uwezeshaji Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu kwa lengo la kuendelea kuwawezesha kiuchumi.
" Zaidi ya Tsh Bilioni 227.9 zinakwenda kusaidia katika kuukuza uchumi kwa watanzania baada ya kurudishwa kwa mikopo ya halmashauri kwaajili ya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu "
Mwenezi Makalla ameyasema hayo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa chama kuanzia ngazi ya mashina, Viongozi wa serikali, Taasisi zisizo za kiserikali, Wazee na Viongozi wa dini katika mkutano maalum wa uwasilishaji wa taarifaya utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa kipindi cha miaka 3 (2021/24) Mkoani Njombe.
Akizungumza katika mkutano huo, Makalla ametoa salamu za shukrani kwa mapokezi makubwa na mazuri pamoja na kufanyika kwa mkutano wa hadhara mkubwa siku ya jana tareghe 18 Aprili, 2024 eneo la Makambako, mkutano ambao amesema ulikuwa wenye maandalizi ya kiwango cha juu.
Aidha, Makalla amesema CCM inaamini Mabalozi wa mashina na mataw ndio wenye watu wanchama wa CCM na wananchi kwa ujumla hivyo kuwataka Mabalozi kuendelea kufanya kazi kubwa wanayoifanya ya kuendelea kuhamasisha na wananchi wengine kujiunga na CCM.
" Tunaamani msingi wa chama chetu ni mabalozi wa mashina na matawi na huko ndipo walipo wana CCM na wananchi, hongereni sana mabalozi kwa kazi nzuri na chama kina imani kubwa nanyi endeleeni kuhamasisha watu kujiunga na CCM "
🗓️19 Aprili, 2024
📍Njombe
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.