Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amesema Mashindano ya Kuhifadhisha Qur-an yana mchango mkubwa katika kuwajenga vijana kimaadili, kifkra na kinidhamu pamoja na kumjua Allah (S.W) na sifa zake
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa mashindano ya Kimataifa ya Qur-an Tukufu uliofanyika katika Ukumbi wa Madinatul Bahar Bweni jijini Zanzibar.
Amesema kuwepo kwa Mashindano ya Qur-an yanawasaidia vijana kujitenga na matendo maovu na macahfu kwa vile hutumia muda mwingi wa kusoma na kujiandaa kushiriki katika mashindano mbali mbali ndani ya nchi na nje ya nchi.
Alhajj Hemed amesema endapo vijana hawatowekewa misingi imara ya kitabia na kuifahamu dini yao watakuwa rahisi kufuata tamaduni za kigeni ambazo zinakwenda kinyumae na mila, silka na desturi za Kizanzibari.
Sambamba na hayo ameikumbusha jamii kuwa kila mmoja ana jukumu la kuhimiza na kusimamia maadili mema kuanzia ngazi ya familia, mashule, madrasa na maeneo ya Ibada ambapo kufanya hivyo kutawasaidia vijana na vizazi vijavyo kuishi katika mazingira ya kumcha Mungu.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na ZBC na Ofisi ya Mufti katika kujenga jamii yenye maadili mame, hivyo Serikali itaendelea kuunga mkono harakati za kidini ambazo dhamira yake ni kuiendeleza dini ya kiislamu na kuimarisha maadili mema ambayo ni nguzo kwa jamii katika kudumisha amani na umoja uliopo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ZBC Bwana RAMADHAN BUKINI ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuridhia na kusaidia kufanyika kwa mashindano hayo jambo ambalo linadhihirisha mapenzi ya viongozi kwa wananchi wake.
Bukini ameeleza kuwa lengo la mashindano hayo ni kuunganisha pamoja Umma wa kiislamu katika mambo ya kheri, kuwaandaa vijana kiroho na kuitambua dini yao sambamba na kupunguza mmong'onyoko wa maadili katika jamii zetu.
Nao wadau wa kuhifadhisha Qur- an wakiongozwa na SHEIKH OTHMAN MAALIM wamewataka waumini wa dini ya kiislam kulipa umuhimu suala la kuhifadhi Qur-an tukufu kwa viajna wao sambamba na kuisoma kwa wingi hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan jambo ambalo linamkurubisha mja na mola wake.
Wamesema mikusanyiko ya kuhifadhisha Qur-an inasaidia kuwabadilisha vijana na jamii kwa ujumla katika kuitambua dini yao ambapo amewaomba viongozi kwa nafasi zao kuunga mkono juhudi zinazofanywa na taasi za Dini kwa maslahi mapana ya Taifa.
Aidha wamewataka watu wenye uwezo kuweza kuzisaidia kwa hali na mali taasisi zenye kuhifadhisha Qur-an kwani kufanya hivyo watapata ujira mkubwa kutoka kwa Allah (S.W) sambamba na kuwataka wafanya biashara kuacha tabia ya kupandisha bei za vyakula hasa katika mwezi wa Ramadhani kwa kutarajia faida mara dufu jambo ambalo ni kinyume na maagizo ya Dini ya kiislamu na Serikali kwa ujumla.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mufti kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji Zanzibar na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar yanatarajiwa kufanyika tarehe 30.03.2024 katika Uwanja wa Amaani Complex Zanzibar na jumla ya Nchi nane (8) zinatarajiwa kushiriki ktk mashindano hayo.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.