Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
HESHIMA KWA MABALOZI NI KUKIRUDISHA CHAMA KWA WANANCHAMA, VIONGOZI NI WATUMISHI TU KWA WANACHAMA - BALOZI DKT. NCHIMBI
> Awapongeza wanaRuvuma kwa kujitoa kimasomaso kwa mapenzi ya dhati kwa CCM
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapiduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewapongeza na kuwashukuru wananchi na viongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa mapokezi nakubwa yaliyoonesha imani kubwa waliyonayo kwa Chama Cha Mapinduzi.
Akizungumza nao kwenye mkutano wa ndani uliokutanisha Viongozi mbalimbali wa Chama , Serikali, Dini, Wazee na Taaasisi zisizo za kiserikali, Balozi Dkt. Nchimbi amewapongeza wanaRuvuma kwa kushinda chaguzi zote zilizopita siku za nyuma hapa karibuni na kuonesha imani yao kutokutetereka kwa CCM na kutoa pongezi kwa ushirikiano wao mkubwa wa Chama na serikali.
" Hongereni kwa uhusiano mkubwa na mzuri wa Chama na serikali na huu ndio unapelekea utekelezaji wa ilani kutekelezwa kwa kasi. "
Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amehimiza juu ya heshima kwa mabalozi kwakuwa ndio msingi imara wa CCM.
" Nilipokuwa mbunge wenu hakuna watu ambao niliwapa heshima kubwa kama mabalozi sababu najua mabalozi ndio msingi wa shina la CCM na ndio maana tumeelekeza nguvu kubwa kuhakikisha Nchi nzima viongozi wote wanatambua hakuna viongozi wakubwa zaidi ya mabalozi na kwa mantiki hiyo chama kitarudi kwa wanachama wengine na sisi tunaochaguliwa na kuteuliwa ni watumishi tu kwa hao wanachama "
🗓️20 Aprili, 2024
📍Songea Mjini - Ruvuma
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.