Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
CCM YATOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA SERIKALI
Katibu NEC itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda ametoa maagizo mbalimbali kwa Mawaziri wa wizara nne hapa nchini ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuwapigia simu mawaziri hao na kutoa majibu ya changamoto mbalimbali.
Mawaziri waliopigiwa simu ni pamoja na waziri wa TAMISEMI Ndugu Mohamed Mchengerwa, Waziri wa mambo ya ndani NduguHamad Massaun, waziri wa uchukuzi Ndugu Makame Mbarawa na waziri wa ujenzi Ndugu Innocent Bashungwa.
Makonda ametoa maagizo hayo leo Novemba 9,2023 wakati akiwa kwenye mkutano wa hadhara akiongea na wananchi mkoani Kagera uliofanyika uwanja wa mashujaa Mayunga.
Moja ya changamoto zilizotajwa ni pamoja na ujenzi wa soko kuu, kingo za mto Kanoni, ujenzi wa stend kuu, uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Bukoba, tatizo la kutopatikana kwa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) maeneo ya mipakani na ujenzi wa barabara za rami ya njia nne kutoka rwamishen junction inayopitia Hamgembe hadi stend kuu ya mabasi Bilele yenye urefu wa kilomita 5.1 ambapo tayari Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshaidhinisha Fedha ya Kuanza Ujenzi wa Barabara Hiyo..
Waziri ofisi ya makamu wa Rais serikali za mitaa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa akijibu kuhusu changamoto za ujenzi wa soko kuu, stend kuu na kingo za mto Kanoni amesema kuwa maagizo ya katibu itikadi na uenezi CCM taifa Makonda ameyapokea na ili kutafanyia utekelezaji haraka mwezi Desemba 2023 atafika mkoani Kagera kwa ajili ya kukagua maeneo itakapotekelezwa miradi hiyo.
Aidha Makonda amewaagiza wakuu wa kitengo cha Usalama barabarani nchi nzima kusitisha kamatakamata zisizo na tija ambazo zimekuwa kero kwa waendesha pikipiki maarufu bodabada.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.