KATIBU MKUU WA CCM AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA IDARA YA UHUSIANO WA KIMATAIFA FRELIMO
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Tawala cha Msumbiji (FRELIMO), Komredi Alcinda Antonio de Abreu, kuhusu masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya Msumbiji na Tanzania, kwa upande mmoja na CCM na FRELIMO kwa upande mwingine, leo tarehe 19 Septemba 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam.