Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar champongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa azma yake ya kuifungua Pemba kiuchumi

alternative

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa azma yake ya kuifungua kiuchumi kisiwa cha Pemba.

Kauli hiyo ameitoa Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi,Zanzibar Khamis Mbeto Khamis kwenye mkutano wa Rais Dk.Mwinyi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu za Majimbo,wilaya na mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema serikali ya awamu ya nane inatarajia kujenga uwanja wa kisasa wa ndege wa Pemba wenye urefu wa mita 2500 katika njia ya kurukia ndege. Katibu huyo alisema mbali na hilo serikali inayoongozwa na Rais Dk.Mwinyi tayari imeshafikisha huduma za umeme kwenye vijiji 65 ambapo kati ya vijiji hivyo vijiji 22 ni kutoka kisiwa cha Pemba. Alisema bajeti ijayo ya serikali itakwenda kukamilisha vijiji vingine vilivyobakia katika kufikisha huduma za umeme."Mheshimiwa Rais katika huduma za maji safi na salama takribani shehia 470 kwa Unguja na Pemba zimefikiwa na huduma hiyo muhimu,"alisema

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor alisema eneo la sekta ya elimu serikali inayoongozwa na Rais Dk.Mwinyi katika kipindi hiki imetengeneza madarasa 158 kwenye mkoa wake ambayopo ndani yake kuna shule tatu za ghorofa na tayari zimekwishaanza kutumika. "Lakini pia mchakato unaendelea ya kuyajenga madarasa mengine kazi imeanza shule  ya Ole,Michakaini na tunatarajia kupata shule ya ghorofa kwenye eneo la kengeja na Wesha,"alisema

Alisema kwa upande wa ajira mkoa wa kusini Pemba imepata ajira mpya 981 za walimu na kwamba bado kuna ajira 500 ambazo zinatarajiwa kupatikana kupitia eneo hilo la sekta ya elimu baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuajiri.

"Katika eneo la miundombinu ya barabara mkoa wetu tunaendelea vizuri tumekamilisha hivi karibuni barabara ya Kijangwani Birikau yenye urefu wa kilomita 4.2 kwa kiwango cha lami na barabara ya Kipapo Mgelema yenye urefu wa kilomita 6.4 imeanza kuwekwa lami,"alisema

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi