Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wakandarasi wanaopewa dhamana ya kujenga Miradi ya Maendeleo Zanzibar kuheshimu Mikataba ya makubaliano wanayokubaliana kati ya Serikali na Kampuni husika
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) lililopo Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo.
Mhe. Hemed amesema kumekuwa na tabia iliyozoeleka kwa baadhi ya wakandarasi kuchelewesha kumaliza kwa wakati miradi wanayopewa kujenga na kuomba kuongezewa muda jambo ambalo linakwamisha adhma ya Serikali ya kutatua kero za wananchi kwa wakati.
Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuheshimu mikataba inayoingia na makampuni mbali mbali pamoja na kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa kampuni zinazojenga miradi ya maendeleo nchini ili kuharakisha ukamilishaji wa miradi hio kwa utaratibu uliopangwa na viwango vyenye ubora.
Makamo wa Pili wa Rais amesema kumalizika kwa wakati kwa ujenzi wa jengo hilo kutatoa fursa kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kufanya kazi zao katika mazingira mazuri na salama kulingana na umuhimu wa ofisi hio.
Sambambana hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kuanzia sasa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) wanapaswa kuwachukulia hatua stahiki Kampuni ambayo haitokabidhi Miradi kwa wakati uliopangwa ili iwe fundisho kwa kampuni nyengine zinazoendelea na ujenzi wa miradi mbali mbali hapa Zanzibar.
Aidha amewataka wakala wa majengo kuacha muhali kwa kampuni yoyote itakayo kwenda kinyume na mkataba wa ujenzi wa miradi ya Serikali ambayo imefungwa baina ya serikali na kampuni husika.
Nae mkandarasi kutoka kampuni ya China Railway Jianhuwang Engineering (CRJE) Chey Yur amesema licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali mwanzoni mwa ujenzi huo lakini watahakikisha wanakamilisha na kukabidhi Jengo hilo ndani ya muda waliokubaliana.
Mkandarasi Yur amesema wameshaongeza nguvu kazi katika ujenzi huo na wanatarajia kuanza kufanya kazi usiku na mchana ili kuongeza kasi ya ujenzi na kukamilisha kwa wakati uliopangwa na kwa ubora zaidi.
Kwa upande wake msimamizi wa Majengo kutoka (ZBA) Mohamed Nahoda Mohamed amesema ZBA wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na Mkandarasi wa ujenzi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 20% ya ujenzi na wanatarajia kukamilisha mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huu.
Ujenzi huo wa Jengo la Ghorofa 4 la Ofisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar utakapokamilika utagharimu zaidi ya Bilioni 11 ambao utajumuisha Ofisi, Kumbi za Mikutano na Vyumba kwa ajili ya wageni
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.