MAKALLA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA VYOMBO VYA HABARI AWAMU YA PILI
Leo Juni 26, 2024 Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Amos Makalla amewataka viongozi na wafanyakazi wa kampuni ya Magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers TSN) kuongeza kasi ya mabadiliko kuingia katika dunia ya Teknolojia.
Ameyasema hayo leo hii alipotembelea ofisi za shirika hilo jijini Dar Es Salaam akihitimisha ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari nchini awamu ya pili.