Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


KATIBU MKUU WA CCM AKITETA JAMBO NA NAIBU WAZIRI MKUU -KATORO GEITA

alternative

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko wakiteta jambo kwa furaha wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Katoro Mjini, mkoani Geita wakati wa ziara ya siku tatu ya Dk Nchimbi mkoani humo Agosti 12, 2024. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita. Nicholaus Kasendamila.

Dk Biteko ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Bukombe mkoani humo, amehudhuria mkutano huo na kujibu baadhi ya kero zilizotolewa na wananchi zinazohusisha wizara ya Nishati. 

Amewahakikishia wananchi wa Katoro kuwa maeneo wanaotaka kuunganishiwa umeme tayari amewaagiza maafisa wa wizara hiyo kwenda kuwaunganishia haraka umeme.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi