Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAMETAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUIOMBEA DUA NCHI PAMOJA NA WAO ILI KUJIKINGA NA MABALAA NA KUPELEKEA SERIKALI KUWEZA KUFIKIA MALENGO ILIYOJIWEKEA
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid AL-ASYIRI Kisauni Wilaya ya Magharibi “B” mara baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Amesema kuwa Dini ya Kiisslamu na dini nyenginezo zinahimiza umoja na mshikamani katika mambo ya kheri hivyo ni wajibu wa Watanzania na wazanzibari kwa ujumla kushikamana katika kuiombea dua nchi yao na viongozi wao ili kuweza kutekeleza ahadi zao za kuwaletea maendeleo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na mikakati ya kupambana na kutokomeza vitendo vya uzalilishaji, utumiaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya nchini ili kuendelea kuwa na Taifa bora lenye kufuata mila, silka na desturi za Kizanzibari ambazo ni urithi kutoka kwa wazee wetu.
Amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar ni waislamu hivyo ni lazima kuishi kwa kufuata maamrisho na makatazo yaliyomo katika kitabu kitukufu cha Qur-an ili kuweza kuwalea watoto wetu katika malezi bora yenye kumpendeza Allah kwa kutambua kuwa kila mtu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga.
Sambamba na haoyo Alhajj Hemed amesema mwezi wa Rajaab hadi kufikia mwezi mtukufu wa Ramadhan ni miezi ambayo waumini wa dini ya kiislamu huvuna mema kutoka kwa Allah, hivyo amewataka waumini hao kudumisha upendo baina yao kwa kutoa walivyonavyo na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum, mayatima na wasiojiweza.
Akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim ALI SHARIF MAALIM amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kushikamana na mafunzo na miongozo ya Allah (S.W) hasa katika malezi ya vijana wetu ili kuweza kupata radhi zake na kufikia malengo ya kuletwa duniani.
Amesema kuwa wazazi na walezi wanawajibu mkubwa sana wa kuwapatia watoto wao elimu zote mbili ili kufikia azma ya Serikali ya kupata wataalamu bora watakao lisaidia Taifa sambamba na kupata wanazuoni wakubwa watakaoitetea dini ya kiislamu.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.