RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa shukurani zake za dhati kwa Jumuiya ya Zawiyyatul Qadiria iliyomuombea dua Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Al hajj Dk. Mwinyi alitoa shukurani hizo baada ya Ibada ya sala ya Ijumaa iliyoambatana na dua maalum ya kumuombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Zanzibar na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, huko Masjid Ngamia Welezo, Mkoa wa Mjini Magharibi. Al hajj Rais Dk. Mwinyi alishukuru Jumuiya hiyo kwa niaba ya familia yake, pamoja na kuwataka waumini wa dini ya Kiislam kuendelea kumuombea dua Marehemu Mzee Mwinyi pamoja na kuliombea taifa ili liendelee kudumu kwenye amani na
utulivu.
“Tuendelee kumuombea dua Mzee wetu, tuendelee kuiombea dua nchi yetu iendelee kudumu kwenye amani tuliyokuwa nayo na Mwenyezi Mungu atupe wepesi katika majukumu yetu” Alisisitiza Al hajj Dk. Mwinyi. Marehemu Mzee Ali Hassan Mwenyi alifariki dunia Febuari 29 mwaka huu, Dar es Salaam na kuzikwa Machi 02, 2024 Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akizungumza kwenye hafla ya dua hiyo, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali mbali na kumpa pole Al haj Dk. Mwinyi kwa msiba wa mzee wake uliotokea hivi karibuni lakini pia alitoa shukurani kwa waislam wote waliohudhuria ibada ya sala ya Ijumaa pamoja na dua maalum ya kumuombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na kuiasa jamii kuongeza ushirikiano kwenye masuala ya kijamii.
Naye Khatib wa ibada ya Sala ya Ijumaa, msikitini hapo aliwataka waumini wa Kiislam kukithirisha sana ibada kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kuendelea kusoma Quran tukufu, kutoa sadaka kwani huweka wepesi wa wamchao Mola, pamoja na kushajihisha jamii kusaidiana kwa kufutarishana hasa kwa wasiokuwa na uwezo kusaidiwa zaidi kipindi hiki.
Sambamba na kuueleza kwamba kila inapofika mwezi Mtukufu wa Ramadhan Mwenyezi Mungu (S.W) huifungua milano yote ya Pepo na kuifunga milango saba ya Moto pamoja na mashetani kufungwa ili kutoa fursa nzuri kwa waumini wa kiislam kufanya ibada kwa uhuru. Akitoa historia ya fupi ya Jumuiya ya Zawiyyatul Qadiria – Tanzania, Mkurugenzi wa huduma nyenginezo wa Jumuiya hiyo, Sheikh Siasa, alisema iliasisiwa mwaka 1988 Tanzania Bara na baadae mwaka 1992 lilifunguliwa tawi lake Zanzibar likiongozwa na mlezi wake Sheikh Said Othman Abdul Kadir Othman bin Muhammed bin Nuur.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025