Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


UFUNGUZI WA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA  JIMBO LA ZIWANI 

alternative

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg Mohammed Said Mohammed (DIMWA) amefungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Jimbo La Ziwani Kilichofanyika katika ukumbi wa Ole Wilaya ya  Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba ..

Ambapo Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed 'Dimwa' amewataka viongozi wa halmashauri kuu ya CCM Jimbo la Ziwani kutoa msukumo mkubwa wa utekelezaji wa ilani ya CCM na kusimamia utekelezaji wa siasa na maamuzi ya CCM kwa ujumla katika jimbo hilo.

Dk. Dimwa aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha halmashauri kuu ya CCM Jimbo la Ziwani, huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba

Alisema, kwa kufanya hivyo watajiletea maendeleo ya dhati bila ya vurugu yeyote katika Jimbo hilo huku akiwahimiza swala zima upendo ndani ya Chama cha Mapinduzi na kuwaasa viongozi wa Jimbo hilo kuanzia ngazi za chini kuacha kuchukiana wenyewe kwa wenyewe.

Alisema, Chama Cha Mapinduzi kinataka umoja na mshikamano kati yao na mapenzi makubwa ili Chama hicho kiendelee kusonga mbele na kupata ushindi katika chaguzi zake zote na kwamba hakuna sababu ya viongozi na wanachama wa CCM wasipendane.

Aidha alieleza kuwa dhamira kuu ya kikao hicho cha halmashauri kuu ya CCM ya Jimbo la Ziwani ni kutekeleza katiba ya Chama Cha Mapinduzi Ibara ya 62 fasili ya pili inayosema, "halmashauri kuu ya CCM Jimbo itafanya mikutano yake kila baada ya miezi sita, lakini inaweza kufanyika mikutano isiyo ya kawaida wakati wowote endapo itatokea haja ya kufanya hivyo".

Hivyo aliwapongeza viongozi wa Jimbo la Ziwani kwa kutimiza kifungu hicho cha 62 fasili ya pili.

Lakini pia alisema, kazi kubwa ya halmashauri kuu ya Jimbo ni kuongoza na kusimamia ujenzi wa ujamaa na kujitegemea katika eneo lake la Jimbo pia kufanya kazi ya uenezi, itikadi na siasa ya Chama Cha Mapinduzi kuelezea mipango ya CCM kwa wadi zote na kubuni mikakati imara.

Alisema, kazi nyengine ya halmashauri kuu ya Jimbo ni kuangalia mwenendo wa siasa na vitendo vya wanachama pamoja na viongozi wa CCM waliomo katika Jimbo hilo na inapolazimu basi kutoa taarifa kwa vikao vya juu.

Alieleza kuwa, dhamira kuu ya kuangalia vitendo hivyo ni usikivu wa maadili wa CCM kwa viongozi kwa kuzingatia nidhamu, audilifu uwajibikaji na lugha zisizokuwa rasmi kwa kuwahudumia wanachama wa Chama cha Mapinduzi.

"Ikiwa kiongozi huna lugha nzuri, ikiwa kiongozi huji kwenye mikutano ipasavyo basi tuachie nafasi yetu manaake huko tayari," alisema

Akielezea majukumu ya vikao hivyo alisema, ni kupanga mikakati ya kampeni za uchaguzi wakati ukifika wa kampeni hizo na kuona kwamba kunakuwepo ulinzi na usalama katika eneo la Jimbo.

Alisema, jambo jengine ni kupokea, kuzingatia na kuamua juu ya mapendekezo ya vikao vya Chama Cha Mpainduzi vilivyopo chini yao mfano wadi na matawi.

Jambo jingine alisema ni kuunda kamati ndogo ndogo za utekelezaji kwa kadri watakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora zaidi wa kazi za Chama Cha Mapinduzi.

"Jingine ni kupokea na kujadili taarifa za kamati ndogo ndogo za utekelezaji wa kazi za Chama Cha Mapinduzi za Jimbo na kamati za mikutano mikuu ya CCM Jimbo letu," alisema.

Lakini Jambo jingine alisema ni kuandaa kamati ya usalama na maadili ya CCM ya Jimbo, na kueleza kuwa ni lazima kamati ya maadili ifanye kazi yake.

Akielezea sababu ya kusisitiza kamati ya maadili kufanya kazi yake Dk. Dimwa alisema, kwa sababu hataki mtu ahukumuwe visivyo katika kamati hiyo na kutaka kila mtu apewe haki yake kwenye jambo hilo.

"Mimi sipo tayari kumdhulumu mtu kwenye Jambo lolote, na viongozi wote walio chini yangu niwamabie tu dhulma haifai na tunatakiwa kuamua maamuzi yaliyokuwa sahihi na tutumie vikao hivi vya maadili kwenye kila ngazi," alisema.

Sambamba na hayo Dk. Dimwa alisema ni matarajio ya Chama hicho kuwa kila kiongozi na mwanachama wa CCM na jumuiya zake ataandaliwa vizuri na kutimiza wajibu wake.

Alisema, utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi utafanikiwa kwa kasi kubwa na nchi itapiga hatua kubwa ya maendeleo kufikia adhma ya Chama Cha Mapinduzi kwa kujenga taifa lililo bora na lenye kujitegemea.

"Kuibua, kuanzisha na kuimarisha miradi ya kiuchumi ya Chama na kulinda mali zote za Chama na Jumuiya zake katika Jimbo letu la zimawani ni katika kukiwezesha chama chetu kujitegemea kiuchumi na mapato kwani utegemezi ni vikwazo vya demokrasia ya vyama vingi," alisema

Pia aliwataka kuandaa mafunzo, semina na madarasa ya itikadi na uongozi katika ngazi mbali mbali za Jimbo hilo na kusema kuwa wakiandaa madarasa ya itikadi ndiyo wataanza kupata wananchama wapya.


Mahali: Mbuzini, Pemba
Tarehe : 17 Febuari, 2024

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi