Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa Shahada ya juu ya Udaktari wa heshima ya uchumi na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki

alternative

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar  Khamis Mbeto Khamis, wakati akizungumza katika mahojiano maalum huko Afisi kwake Kisiwandui Zanzibar.

Amesema heshima hiyo ni kubwa na inadhihirisha uhodari,uchapakazi,ubunifu na ueledi wa Rais Dkt.Samia katika kupaisha uchumi wa Tanzania katika nchi za Afrika zinazopiga hatua kubwa za maendeleo kiuchumi.

Mbeto,alisema CCM Zanzibar imepokea kwa furaha kubwa taarifa za kupewa heshima hiyo kubwa ya shahada ya Juu na Chuo chenye hadhi kubwa ya kufundisha fani za masuala ya uchumi duniani kilichofanya utafti wa kina na kikajiridhisha na kutoa heshima hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Chama Cha Mapinduzi tunampongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupewa heshima hii ya Shahada ya Juu ya Phd hakika utendaji wako uliotukuka umeonekana hata kwa mataifa ya mbali hivyo nasi wananchi wake tuendelee kumpa moyo na kumuunga mkono.”,alisema Mbeto.

Katika maelezo yake Mbeto,amefafanua kuwa mara nyingi heshima hiyo ya udaktari hutolewa kwa mtu au kiongozi aliyeonyesha juhudi na mchango mkubwa katika Taifa lake katika kuivusha nchi katika mambo magumu yanayobeba maslahi mapana ya taifa kwa ujumla.

Alisema maono,busara na falsafa za Rais Dkt.Samia za kufungua milango ya diplomasia ya kiuchumi kwa mataifa mbalimbali kuja nchini kutembea na kufanya uwekezaji huru na wenye tija vinaendelea kumg’arisha kiuchumi katika anga za kimataifa.

Katibu huyo wa NEC, Mbeto, alitoa wito kwa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Wananchi kwa ujumla kuendelea kumuombea dua ili Mwenyezi Mungu ampe Rais Dkt.Samia nguvu,ujasiri na maamuzi sahihi ya kufanikisha mipango ya kuwaletea wananchi wote maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Sambamba na hayo Mbeto, alikumbusha kwamba Dkt.Samia tayari ametunukiwa shahada nne za heshima toka ameingia madarakani Machi 19,2021 ambazo ni Shahada ya kwanza ya heshima ya udaktari,aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es saalam(UDSM) mwaka Novemba 30,2022.

Nyingine ni Shahada ya heshima ya Udaktari wa  Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru nchini India, Oktoba 10,2023, heshima ya Udaktari ya usimamizi wa Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Disemba 28, 2023 pamoja na aliyoipata jana ya Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki.

alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi