MAKALLA AKABIDHIWA UCHIFU WA WANGINDO
LINDI: KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amekabidhiwa uchifu wa Wangindo alipofika katika Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya tamaduni za wangindo.
Makalla alipewa nafasi hiyo ya uchifu na kuvalishwa vazi la kuashiria tamaduni hizo Aprili 11,2025 alipofika kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa Wilaya hiyo ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya siku 10 katika mkoa wa Lindi na Mtwara.