KATIBU MKUU WA CCM AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey, kuhusu masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya India na Tanzania, leo tarehe 19 Septemba 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam.