Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Dk. Hussein Ali Mwinyi amelipongeza Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya Afya na quot AMREF heath Africa Group and quot; kwa kufanikisha mkutano wao hapa Zanzibar uliowashirikisha Mawaziri wa Afya kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika
Rais Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo Ikulu, Zanzibar alipotembelewa na uongozi wa Shirika hilo ulioambatana ujumbe wa Mawaziri hao kwa lengo la kumpa pole baada ya kufiwa na baba yake mzazi hivi karibuni, Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais
Mstaafu wa Zanzibar na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Dk. Mwinyi amesifu hatua ya mkutano huo kushirikisha mataifa mbalimbali ya Afrika na kujadiliana masuala ya Afya na changamoto za Afya zinazoikumba Afrika.
Alisema, Shirika la & quot; AMREF health Afrika & quot; ni mdau muhimu kuwahi kufanyakazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye Sekta ya Afya. Pia, Rais Dk. Mwinyi ameeleza ushirikiano wa karibu uliopo baina ya & quot; AMREF Tanzania & quot; na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na kuongeza kuwa Shirika hilo, limekua likiungamkono juhudi za Serikali kwa misaada mbalimbali, vifaa, mafunzo na kubadilisha uzoefu kwenye masuala ya Afya kwa lengo la kuboresha Sekta ya Afya, Zanzibar. Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameushukuru ujumbe huo kwa kumfariji kutokana na msiba wa kufiwa na Baba yake mzazi hivi karibuni.
Naye, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo la AMREF Health Africa Group, Dk. Githinji Gitahi, amemueleza Rais Dk. Mwinyi adhma ya kuwepo kwao Zanzibar baada ya kufanikisha mkutano wa kimataifa wa Mawaziri wa Afya kutoka Afrika ambao walifanikiwa kujadili na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha Sekta ya Afya, Afrika pamoja na kuzibiti magonjwa mbalimbali ikiwemo maradhi ya malaria na magonjwa yasiyoambukiza.
Aidha, Ofisa huyo alieleza namna ya & quot; AMREF health Afrika Group & quot; inavyofanyakazi Afrika. Wakati huo huo, Mkurugenzi wa & quot; AMREF - Tanzania", Dk. Florence Temu, alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Shirika hilo limekua na ushirikiano wa karibu na Serikali zote nmbili ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. AMREF Tanzania inafanya kazi kwa karibu na taasisi za umma na binafsi pamoja na mashirika ya Serikali, wafadhili, mashirika ya kijamii na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.