Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema uwepo wa Maonesho ya Wiki ya elimu ya juu nchini yamekuwa yakiziweka pamoja Taasisi, vyuo na wadau wa elimu ya juu kwa lengo la kutangaza fursa mbali mbali kwa wanafunzi wanaosoma na wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu vya ndani na nje ya Nchi

alternative

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Tano(5) ya wiki ya elimu ya juu Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mhe. Hemed amesema kupitia maonesho ya wiki ya elimu ya juu wanafunzi hupatiwa fursa mbali mbali za kimasomo ikiwemo upatikanaji wa mikopo, namna ya kujiunga na vyuo vya ndani na nje ya nchi na kutoa hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii na kujiendeleza katika ngazi ya elimu ya juu.

Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Sera na Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imekuwa ikichukua hatua mbali mbali za uboreshaji wa elimu  ikiwemo kuweka mageuzi makubwa  kuanzia ngazi ya maandalizi hadi elimu ya juu kwa kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi na maarifa baada ya kumaliza masomo yao.

Aidha Serikali imeongeza Bajeti ya Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu Zanzibar kutoka fedha za Kitanzania shilingi Bilioni 26.95 kwa mwaka wa fedha 2024 hadi kufikia Bilioni 30.5 kwa mwaka 2025 ambazo zitakwenda kuwanufaisha wanafunzi zaidi ya 7,367 ambapo kwa mara ya kwanza wanafuzi 1,000 wa ngazi ya Diploma watanufaika pia na mikopo hio.

Amefahamisha kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ikiwemo kuwapatia Bima ya Afya pamoja na kuongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wote  wanaosoma Vyuo vya Zanzibar na vyuo vya Tanzania Bara.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametoa wito kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla kujitokeza na kuitumia vyema wiki ya maonesho kwa kujielimisha juu ya upatikanaji wa fursa mbali mbali za elimu ndani na nje ya nchi na kuwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidiii na kuzitumia vyema fursa wanazozipata pamoja na kuepuka kutumika kwa misingi yoyote ambayo itapelekea kuvuruga umoja na amani iliyopo nchini

Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussen Mwinyi inafanya kazi kubwa na nzuri katika kuimarisha miundombinu ya elimu inayopelekea kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu jambo ambalo linaendelea kuiletea heshima zanzibar.

Mhe. Lela amesema ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha sita unaongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia asilimia 99.5% kwa mwaka 2024, ambapo zaidi ya wanafuzi 3,387 wamepata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu na wote wanatarajiwa kujiunga na vyuo vikuu mbali mbali ndani na nje ya nchi, hivyo kupitia  maonesho ya juma la elimu ya juu yatawasaidia katika kufanya udahili wa vyuo na kupata taaluma juu ya kupata mikopo ya elimu juu iatakayowawezesha kusoma pasipo na changamoto ya aina yoyote.

Akisoma taarifa ya kitaaluma kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Naibu katibu Mkuu Utawala (WEMA) Khalid Massoud Waziri amesema lengo kuu la maonesho hayo ni kuimarisha mashirikiano baina ya Taasisi za Elimu, Vyuo na Mabenki ili kuhakikisha Sekta ya Elimu nchini inaendelea kuimarika na kiwango cha ufaulu kuzidi kuongezeka siku hadi siku.

Khalid amesema maonesho hayo ya juma la Elimu ya juu yanazidi kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka huu washiriki wameongezeka kutoka washiriki 17 mwaka 2020 hadi washiriki 77 mwaka 2024  na kutoa fursa kwa wanafunzi kupata kujua ni namna gani wanaweza kujiunga na vyou vikuu vya ndani na nje ya nchi samabamba na kupata kujua ni namna gani mwanafuzni anapata fursa ya kufanya maombi ya mikopo kwa taasisi husika.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametembelea Mbanda ya washiriki wa maonesho  ya juma la Elimu ya juu na kupata elimu na huduma zinazotolewa katika mabanda hayo

alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi