Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


KUTOKA WILAYA YA MPWAMPWA, MKOANI DODOMA.

alternative

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Dodoma Ndugu Lailah Burhan Ngozi (MCC) , ameendelea na ziara ya Kujitambulisha na Kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi kwa Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025, Kutembelea Mashina na kufanya Mikutano ya ndani.

Aidha  Ndugu Lailah Burhan Ngozi ambaye pia ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma amewaeleza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi  ukiwa ni muendelezo wa ziara yake Wilayani Mpwampwa kuwa Miradi mbalimbali inayotekelezwa ni pamoja na Miradi wa Miundombinu ya Barabara, Elimu, Afya na Miradi ya Kijamii.

Pamoja na hayo, Ndugu Lailah Burhan Ngozi (MCC), ameupongeza Uongozi wa CCM wilaya ya Mpwapwa kwa kuweza kuondoa makundi yaliyojiyokeza wakati wa Chaguzi  zilizopita

Mwisho, Wananchi na Wanachama wamepongeza Ziara ya Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, wamesema Ziara ya Mlezi  imechangia kuleta  matumaini ya utatuzi wa upatikanaji wa huduma ya Maji na Salama  kwa Wakaazi wa Kata ya Mazae  ambayo yamekosekana  kwa muda  mrefu.

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi