Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
CCM YAIOMBA SHIRIKA LA KTI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE
Katibu wa NEC Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (MCC) Ndg. Rabia Abdallah Hamid, Septemba 19, 2024 Chini Uingereza amefanya mazungumzo na Bw. Will Straw, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kings Trust International (KTI) na kuiomba Taasisi hiyo kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwawezesha vijana na wanawake.
Aidha, Ndugu Rabia amewasilisha ombi kwa Taasisi hiyo kuona uwezekano wa kuanzisha mashirikiano na Tanzania hususani kwa ajili ya programu za kuwezesha wanawake.
Alieleza kwamba, uwezeshwaji vijana ni moja wapo ya ajenda ya kipaumbele ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi.
Ameongezea kwamba, katika kuendeleza uchumi wa vijana na wanawake Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya jitihada kubwa kuwezesha vijana na wanawake kupitia programu mbalimbali kama vile utoaji wa ardhi kwa vijana na kuwapatia ruzuku kujishughulisha na kilimo; kuwapatia vifaa salama vya
uvuvi ili kukuza uvuvi endelevu; kuwapatia vifaa vya kupikia kama vile majiko ya gesi ili kujilinda na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Taasisi hiyo inajishughulisha na kuwezesha vijana kupata ujuzi mbalimbali ili waweze kuingia kwenye soko la ajira. KTI, ilianzishwa mwaka 1976 na Mwana wa Mfalme, Charles ikiitwa kama Prince’s Trust na imekuwa ikifanya kazi hizo za kuhamasisha mafunzo mbalimbali kwa vijana ili kukuza vipaji vyao na kuwawezesha kupata ujuzi mbalimbali katika masuala
ya biashara, ujasiriamali, ubunifu na teknolojia.
Mwaka 2015, Taasisi hiyo ilipanua wigo wa huduma zake na kuanza kufanyakazi katika nchi 25 za Jumuiya ya Madola (JYM). Hivyo, ilibadilishwa jina na kuitwa Prince Trust International (PTI). Kupitia program zake, Taasisi hiyo imeendelea kuwawezesha vijana kujitegemea na kuchangia maendeleo ya jamii wanazoishi. Mwezi Julai 2024, Taasisi hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa Kings Trust International (KTI) kufuatiwa kutawazwa kwa Mfalme Charles III wa Uingereza.
Kupitia Mkutano huo, Bw. Straw amemueleza Ndg. Rabia kazi zinazofanywa na Taasisi
yao ya kuwasaidia vijana kupata ujuzi na ufundi wa ziada ya mafunzo ya darasani.
Ameongezea kwamba vijana hao kupitia mchezo wa Enterprise Challenge wanafundishwa
kubuni mawazo ya kibiashara ambayo baadae hushindanishwa na washindi kupewa mitaji midogo ya kuweza kutekeleza miradi au biashara walizobuni.
Aidha ameongezea kwamba, nchini Tanzania, Taasisi hiyo inafanyakazi na Asante Africa Foundation kupitia After School Clubs katika shule 20 nchini, ambapo wanafunzi wanapewa vifaa kama computers, laptops na kupatiwa mafunzo ya ubunifu wa mawazo ya biashara.
Lengo la kuwapatia ujuzi wa ziada ni kuwawezesha kuingia katika soko la ajira.
Pamoja na hayo Taasisi hiyo inafanya kazi na Mo Dewji Foundation kusaidia vijana kupata ujuzi kupitia mitaala inayoendanana soko la ajira ya sasa na utaalam wanaopata unasaidia kupata ufadhili wa masomo kupitia scholarships.
Vilevile, ameelezwa kwamba KTI ipo katika mazungumzo
na Benk iza CRDB na NMB kwa lengo la kushirikiana katika kuwezesha vijana wa
Kitanzania kupata ujuzi wa ujasiriamali, ufundi, ubunifu, teknolojia na kuweza
kujitegemea na kuchangia katika uchumi wa nchi.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.