RAIS WA ZANZIBAR DKHUSSEIN ALIMWINYIAMEKUTANA NA UJUMBEKUTOKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA ELIMU SAYANSI NA UTAMADUNI (UNESCO) KUJADILI MASUALA YA UTUNZAJI WA HIFADHI YA MJI MKONGWE
Dk. Mwinyi alikutana na ujumbe huo Ikulu, Zanzibar ukiambata na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said pamoja na maafisa wa Wizara hiyo.Alisema, licha ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa na Zanzibar bado Urithi wa hifadhi ya kimataifa ya Mji Mkongwe unaendelea kulindwa na kuenziwa kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizowekwa. Rais Dk. Mwinyi aliueleza ujumbe huo kwamba, Selikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imechukua hatua mbalimbali za kuutunza urithi ikiwemo kuondosha msongamano wa maegesho ya vyombo vya moto kwenye maeneo yote ya Mji Mkonge wa Zanzibar, ili kuenzi haiba ya mji huo kuendelea kuwa kivutio mashuhuri cha watalii
na wageni wanaoutembelea mji huo. Aidha, alisema katika kutekeleza hatua hiyo, Serikali imeamua kujenga maegesho ya vyombo vya moto eneo la Darajani ikiwa njia mbadala ya kuondosha msongamano wa magari kwenye maegesho ya Mji Mkongwe.
Pia Dk. Mwinyi, aliueleza Ujumbe huo kwamba hatua nyengine iliyochukuliwa na Serikali ni kushirikiana na sekta binafsi kuutunza Urithi huo hasa kuyaendeleza majengo yaliyochakaa kwa kuyakarabati kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kuyaenzi majengo hayo kuyarudisha kwenye uhalisia wake. Alisema, Serikali inasimamia kwa karibu na kuhakikisha thamani na mali zote za asili zilizokuwemo kwenye majengo hayo zinarudishwa sehemu husika baada ya ukarabati.
Akizungumzia jengo la Beit el Ajaaib na la People’s Palace, Rais Dk. Mwinyi aliueleza ujumbe wa UNESCO kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman wanaendelea kusimamia ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, Dk. Mwinyi alieleza Beit el Ajaaib na la People’s Palace ni alama muhimu inayoitambulisha Zanzibar duniani kote.
Nao, Ujumbe huo wa UNESCO, uliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuendelea kuuenzi na kuutunza urithi huo ili kuunusuru na athari za mabadiliko ya teknolojia ikiwemo kukua kwa maendeleo ya nyanja mbalimbali nchini ambayo kwa namna moja ama nyengine itakua sababu ya kubadili mandhari halisi na mwonekano wa mji huo.
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
01-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆’-𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀
01-06-2026
𝐍𝐈 𝐍𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀!
01-06-2026
🔰𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎!
01-06-2026
𝐒𝐇𝐔𝐋𝐄 𝐘𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐒𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐌𝐄𝐓𝐀 𝟏𝟐 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈
01-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐈, 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐀𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
𝐍𝐈 𝐌𝐔𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐇𝐀𝐈-𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐒𝐀𝐒𝐀
01-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
01-06-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
01-06-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
01-06-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
01-06-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
01-06-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
01-06-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
01-06-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
01-06-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
01-06-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
01-06-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
01-06-2026