MAKALLA: CCM ITAENDELEA KUTATUA KERO ZA WANANCHI
•Aongea na wananchi DUMILA na kusikiliza kero
DUMILA: Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi(CCM) CPA, Amos Makalla amesema chama hicho, ndicho chenye jukumu la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Watanzania..
CPA, Makalla amesema wajibu huo unatekelezwa vema na CCM, akiwataka Watanzania kutokuwa na wasiwasi kuhusu utatuzi wa kero zinazowakabili kwa sababu maendeleo yanaendana na changamoto.
CPA, Makalla ameeleza hayo leo katika Kata ya Dumila wilayani Kilosa aliposimama kuwasalimia wananchi wa eneo akieleke wilayani Gairo kufanya mkutano wa hadhara.
"CCM ndio yenye thamana ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wengine hawawezi hilo," amesema CPA.
Katika mkutano huo, Makalla alizibeba kero za maji, barabara, ushuru na stakabadhi gharani zilizowasilishwa na wananchi wa Dumila aliyewapa fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili.