Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
HODI SIMIYU, NCHIMBI AKIANZA ZIARA YA SIKU 3
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa Lamadi, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu, leo tarehe 6 Oktoba 2024, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Balozi Nchimbi ambaye ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Makalla na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (Suki), Ndugu Rabia Hamid Abdalla, ameanza ziara mkoani Simiyu kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kukagua uhai wa Chama kuanzia ngazi ya mashina na pia kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika mwezi Novemba, mwaka huu.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.