Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


HADI SASA TUMEFANYA MIKUTANO 30 NA KERO 148 ZIMESHATOLEWA UFUMBUZI - MWENEZI MAKALLA

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Amos Makalla, amesema hadi kufikia sasa kupitia ziara hii ya Katibu Mkuu kutembelea mikoa sita, tayari imefanyika jumla ya mikutano 30 na vikao sita vya kamati ya siasa ambapo ahadi kubwa iliyotolewa na wananchi ni kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi wa mwaka 2025.

Mwenezi Makalla amesema wananchi wamekihakikishia Chama kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na kuzoa viti vya ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu.

“ Katika ziara hiyo ya mikoa sita kazi kubwa imefanyika, tulianza ziara mkoa wa Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma kwa awamu ya kwanza ambako kote tulipopita tumepokelewa kwa kishindo. Tumefanya mikutano 30, vikao sita vya kamati ya siasa, tumeangalia uhai wa Chama na kote tulipopita wameahidi mambo mawili kuhusu uchaguzi" .

Makalla ameeleza mambo hayo ni;
" Kwanza CCM itashinda kwa kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa, wameahidi madiwani na wabunge tutashinda kwa kishindo lakini nafasi moja ya urais fomu yake ni moja tu ya Rais Samia. Mikoa yote inasimama na Rais Samia, ahadi kubwa ni ushindi kwa CCM .”

Akizungumza kwenye mkutano wa ndani, Mwenezi Makalla amesema hadi kufikia juzi jumla ya kero 148 zimesikilizwa na kutolewa ufumbuzi huku akitumia nafasi hiyo kuwaagiza viongozi wa CCM kusikiliza kero za wananchi kisha kuzifikisha serikali kwa ufumbuzi.

“ Ofisi za CCM ni kimbilio la wananchi, wasikilizeni wananchi kisha kero zao mzipeleke katika ofisi za serikali, msiwaachie watendaji wa serikali peke yao ,” alisema Mwenezi Makalla

Vilevile, Mwenezi Makalla ameendelea kusisitiza juu ya uwepo wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri mahususi kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.

“ WanaCCM na jumuiya zote tuhamasishe wenzetu wanufaike na mikopo hiyo kwa sababu wapinzani kwao siyo ajenda. Wapo kwenye maandamano na wanaamini vijana wao wakiwa masikini ndiyo watawatumia kwenye maandamano" .

🗓️22 Aprili, 2024
📍Mbinga - Ruvuma

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi