KINANA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KUFUATIA KIFO CHA RAIS WA NAMIBIA DKT. HAGE G. GEINGOB
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg. Abdulrahman Kinana amesaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Namibia Hayati Mheshimiwa Dkt. Hage G. Geingob. Ndg Kinana amesaini Kitabu hicho katika Ofisi za Ubalozi huo uliopo Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Februari, 2024.