Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
ALHAJJ.DKT HUSSEIN ALI MWINYI AMESEMA NIDHAMU, UADILIFU NA UWAJIBIKAJI NDIO SUALA LA MSINGI NA MUSTAKABLI MWEMA KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA TAASISI BINAFSI KWA KUTARAJIA RADHI KUTOKA KWA ALLAH (S.W)
Ameyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ALHAJJ HEMED SULEIMAN ABDULLA katika Kongmano la TISA (9) la kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar.
Alhajj Dkt Mwinyi amesema kuwa dini ya Kiislam imehimiza suala la uwajibikaji na ufanisi kwa kila mtu kwani ndani yeke hupatikana maendeleo kwa mtu moja moja na taifa kwa ujumla.
Aidha amewakumbusha waumini wa dini ya kiislamu juu ya umuhimu wa suala uadilifu sio la viongozi tu kwa raia zao bali hata raia anapaswa kumfanyia uadilifu mwenzake kwani kufanya hivyo kutapelekea mapenzi makubwa baina yao.
Sambamba na hayo Alhajj Dkt Hussen Mwinyi amewataka wafanya biashara wakubwa na wadogo kuwafanyia tahfif wananchi katika kuwauzia bidhaa mbali mbali ili kila mmoja aweze kujikimu na maisha hasa katika Mwezi wa Ramadhani ambao unafadhila nyingi ndani yake.
Amesema kwa upande wa Serikali itahakikisha bidhaa za vyakula zinapatikana nchi nzima na zinaingia kwa wakati sambamba na kufuatilia na kusimamia bei elekezi zilizotolewa na Serikali ili kuwasaidia wananchi kuweza kufunga kwa salama na kupata futari kwa wakati bila ya usumbufu wowote.
Akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Wa Katiba Sheria Utumishi Na Utawala Bora Mhe. HAROUN ALI SULEIMAN amesema umefika wakati taasisi kuzihifadhi hutuba zote zinazotolewa na viongozi wakiwemo viongozi wa dini kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae.
Amesema kuhifadhiwa kwa hutuba zinazotolewa na Mashekhe hasa katika makongamano ya dini kutazisaidia sana jamii kuweza kujifunza na kuwaenzi wanazuoni hao pindi watakapokuwa wametangulia mbele ya haki.
Akitoa salamu kutoka ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar KATIBU MTENGAJI kutoka ofisi hio SHEH HALID ALI MFAUME amesema Ofisi itaendelea kutoa miongozo kwa taasisi zote za kidini kwa lengo la kuupeleka uislamu mbele pamoja na kulinda mila na silka za wazanzibari ambao wamerithi kutoka kwa wazee wetu.
Sheh Halid amesema ni lazima waumini kuendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi wakuu wa nchi za kuwaletea maendeleo wananchi wake sambamba na kuwaombea dua hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhan ili kuweza kutimiza yale yote walio yaahidi kwa wananchi kwa faida ya sasa na baadae.
Mapema Katibu wa Taasisi ya ZANZIBAR WELCOMING RAMADHAN CONFERENCE ambao ndio waandalizi wa kongamano hilo linalofanyika kila mwaka Ndugu ALI MOH’D HAJI amesema taasisi huandaa kongamano hilo kwa lengo la kuwakumbusha waumini wa dini ya kiislam juu ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kufanya yale yote yanatakiwa kufanywa sambamba na kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na serikali kuu.
Hata hivyo ametowa wito kwa viongozi wa serikali na wa sekta binafsi kuwajibika ipasavyo katika kutoa haki kwa kila mwananchi kwani kufanya hivyo ndio kutapelekea kuupeleka mbele uislamu sambamba na kumsaidia kwa vitendo rais wa Zanzibar na rais wa jamuhuri ya muungano kufikia malengo waliojiwekea kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao watoa maaada katika kongomano hilo wamewaasa waumini wa dini ya kiislamu kuwatii na kuwahashimu viongozi wa nchi kwa dhamana zao walizonazo sambamba na kuthamini jitihada zao wanazozifanya katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Wamesema waislamu wanapaswa kujisahihisha katika uwajibikaji kwa kuwa wadilifu katika maeneo yao ya kazi na hata katika jamii zinazowazunguka kwa kutendeana haki, kushajihishana katk kutenda mema na kukatazana mabaya ili kuweza kupata Radhi za Allah hasa katika mwezi Mtuku wa ramadhani.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.