Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kuendeleza  ushirikiano katika kazi utakaoleta manufaa makubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku

alternative

Akifungua kikao kazi kati ya Mahakama ya Tanzania, Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar na Mfuko wa  Fidia kwa wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Zanzibar Beach Resort,  Mhe. Hemed amesema Taasisi hizo zinapaswa kuwa na maazimio ya pamoja katika kuzifanya maboresho mbali mbali sheria zote zinazohusiana na malipo ya fidia kwa wafanyakazi na taratibu zote zinazotumika katika kutoa huduma hio.

Mhe. Hemed amesema waajiri wote Tanzania Bara na Zanzibar wanapaswa kubeba dhamana kwa wafanyakazi wao pindi wanapopata majanga yatokanayo na kazi kwa kuchukua hatua za haraka ikiwemo kutoa taarikwa kwa WCF na ZSSF ndani ya muda uliowekwa kisheria ili wafanyakazi au  wategemezi wao waweze kupata mafao stahiki kwa wakati.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema uwepo wa Majaji wa Mahkama  Kuu kwa pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao kazi hicho kinatoa fursa kwao kujifunza namna  ya kufanya kazi na WCF pamoja na ZSSF  hasa katika kuboresha huduma za kimahakama kwa kutambua hatua mbali mbali katika uchakataji wa madai ya wafanyakazi waliopata madhila yatokanayo na kazi wanzozifanya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewahakikishia washiriki wa kikao kazi hicho kuwa Serikali zote mbili zitaendelea kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuboresha mahusiano yenye lengo la kuleta ustawi wa wafanyakazi pindi wanapokuwa kazini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana na watu wenye ulemavu MERY MAGANGA amesema vikao kazi kama hivi vinaumuhimu mkubwa sana katika kudumisha Muungano wa Tanzania pamoja na kuimarisha utendaji kazi kwa wafaanyakazi jambo ambalo huleta tija kubwa kwa Taifa.

MAGANGA amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya pande zote mbili za Muungano kwa kuhakikisha sheria ya fao la Fidia linatekelezwa kwa haki na usawa kwa wafanyakazi wote sambamba na kuwataka washiriki wote wa kikao hicho kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo yale ambayo watakubaliana katika mkutano huo.

Nae Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. MUSTAPHER  SIYANI amesema lengo kuu la kikao kazi hicho kufanyika Zanzibar ni kudumisha Muungno na kuweka mazingira bora na rafiki yenye kuvutia wawekezaji hasa pakiwa na mfumo Imara wa utowaji na upatikaniji wa haki nchini.

SIYANI amesema kikao hiki kitawakumbusha Majaji, watendaji wa mahakama  na wadau wa haki juu ya utekelezaji wa nguzo ya pili ya upatikanaji wa haki na kuwasaidia katika kutafuta utatuzi wa migogoro ya kazi katika Taasisi mbali mbali zilizopo nchini.

Mapema  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. JOHN MDUMA amesema Utiaji wa saini wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja kati ya WCF na ZSSF unathibitisha mahusiano imara waliyonayo kwa muda mrefu yanayodhihirisha utayari wa kuwasaidi wafanyakazi hasa pale wanapopata majanga wakiwa kazini.

Dkt. MDUMA amesema WCF wameona ipo haja na umuhimu wa kuwajengea uwezo Wazanzibari katika kuzifahamu vyema huduma za mafao ya fidia kazini ili kuweza kutoa haki kwa mfanyakazi ama wategemezi wao pindi mfanyakazi atakapopata ajali akiwa kazini.

Katika kikao hicho Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ameshuhudia utiaji wa saini kati ya WCF na ZSSF ya makubaliano ya kufanya kazi kwa ushirikiano jambo ambalo litaleta tija na mafanikio makubwa kwa wafanya kazi wa pande zote mbili za jamuhuri ya muungano wa Tanzania

alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi