Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MAKONDA: KILA MWANANCHI ATOE MAONI YAKE KUHUSU DIRA YA MAENDELEO

alternative

KATIBU wa Itikadi na Uenezi  Paul Makonda amewataka wananchi  kujitokeza kwa wingi katika suala zima la utoaji wa maoni ya dira ya Maendeleo ya Taifa ya  miaka 30.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kutoa tathmini ya robo mwaka ya chama cha mapinduzi Makonda amesema kuwa tayari sheria imeshapitishwa na  bunge hivyo ni jukumu la kila Mwananchi kutoa maoni ya nini anataka kiwekwe katika dira hiyo.

"Niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi katika suala zima la utoaji wa maoni ya nini wanachotaka kiwekwe, na mpango huu utawafikia wananchi wote kwa sababu tayari tume maalum imewekwa kwa ajili ya kukusanya maoni hayo',amesema Makonda.

Katika hatua nyingine katibu huyo amekerwa na kitendo cha ukatikaji wa umeme Mara kwa Mara Na kuwataka viongozi wa Tanesco kujitathminib wenyewe bila kusubiri kushurutishwa.

Amesema hivi karibuni Tanesco wamemuahidi Rais Samia ya kwamba ifikapi Januari kuwa kinu cha umeme kitawashwa hivyo ni vyema ahadi hii ikatekelezwa kwa vitendo.

Aidha amewataka watendaji wote kuanzia ngazi shina hadi mkoa kusikiliza kero za wananchi Ila kutatua changamoto zinazowakabili.

" Nataka niwakumbushe ndugu viongozi tuliopewa dhamana Na Rais Samia ya kuwatumikia wananchi ni vyema tukatekeleze wajibu wetu tusisubiri mpaka Rais Samia anzishe ziara aanze kasimamishwa njiani na wananchi ili watoe malalamiko yao,"amesema Makonda.

Akizungumzia suala la kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa Makonda amesema ni vyema wanachama wenye nia ya kugombea uongozi kuacha viongozi waliopo madarakani waendelee kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wao bado ni viongozi Halali wanaotambulika kisheria.

"Najua wapo watu ambao wameanza kampeni za hapa Na pale Mimi niwambie tu ndugu zangu waacheni viongozi wafanye kazi kwa sababu muda wao haujaisha Na wao bado ni viongozi wanaotambulika na bado wanahaki ya kuwatumikia wananchi", amesema Makonda.

Hata hivyo Pauli Makonda  amebainisha kuwa kuanzia Januari 13 /2024 ataanza ziara ya kikazi katika mikoa 10 ikiwemo  Tanga,Pwani,Kilimanjaro,Arusha,Manyara,Singinda,Tabora,Shinyanga  na Simiu.

Ambapo amewataka watendaji wa halmashauri zote watakaopitiwa na ziara hiyo waanze kujitathmini kabla ya kiongozi huyo kupita maeneo hayo.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi